Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya
******
MWENYEKITI
wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa
Iringa mwanahabari Tumain Msowoya ametishia kujiuzulu nafasi yake hiyo
baada ya wajumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa kupinga uamuzi wake wa
kuchomoka ajenda ya kumteua mume wake kuziba nafasi tano ambazo anapaswa
kuteua kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM.
Msowoya
alifikia uamuzi huo wa kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo jana katika
baraza kuu ya UVCCM mkoa lililofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa
Iringa . Kamujibu wa kanuni ya UVCCM ilipaswa ateue wajumbe watano wa
baraza la UVCCM mkoa ambapo wajumbe wanne alikwisha teua katika baraza
la vijana lililofanyika Desemba 8 mwaka 2012 hivyo kubaki nafasi moja
ambapo jana
alipaswa kuiziba nafasi hiyo
na kumteua mume wake Frank Kibiki aliyekuwa katibu wa UVCCM Iringa
vijijini ambae kwa sasa yupo rikizi. Hata hivyo wajumbe walionyesha kuwa
na maswali mengi kuliko majibu ya kuhoji hasa ukizingatia katibu wa
wilaya ni mjumbe halali wa baraza kuu la mkoa hivyo hapaswi kuteuliwa
nafasi nyingine kuwa mjumbe mara mbili hali wanachama wengine wapo .
Hivyo wajumbe walihoji sababu
ya mwenyekiti wao huyo kuingiza ajenda ya uteuzi wa nafasi hiyo moja
ambayo mwanzoni haikuwepo katika ajenda za baraza hilo na kumtaka
kusubiri baraza lijalo jambo ambalo ajenga hiyo ingeingizwa na si
kuchomekea katika baraza hilo.
hatua hiyo ilimfanya
mwenyekiti huyo kuingiwa na jazba na hivyo kutangaza kujiuzulu nafasi
yake huku akitoka nje ya ukumbi na kupelekea kamati ya utekelezaji ya
mkoa kumfuata nje ya ukumbi na kumwolekeza kanuni zinasemaje juu ya
uteuzi na namna ya ajenda kujulikana kwa wajumbe na baada ya hapo
aliingia ndani ya ukumbi na kurejea kauli yake ya kujiuzulu na kutoka
kabisa eneo la mkutano kwa hasira huku akisisitiza kuwa hakushinikizwa
na mtu kujiuzulu nafasi hiyo bali ni maamuzi yake binafsi .
Hata hivyo jazba ya mwenyekiti huyo ilitulizwa na wajumbe wa baraza hilo waliopinga uamuzi wake huo.
“Hatukubaliani na uamuzi
aliotaka kuuchukua; hawezi kuucha umoja wa vijana katika kipindi hiki
ambacho chama kinaelekea kwenye chaguzi ndogo tatu za udiwani mkoani
hapa,” alisema mmoja wa wajumbe katika baraza hilo
Aidha mjumbe huyo alisema
Msowoya hawezi kujiudhulu nafasi yake hiyo kwa jazba kutokana na kile
alichokiita ‘majungu’ yanayopikwa na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo.
“
Kilichopelekea atishie
kujiuzulu ni pamoja na majungu yanayopikwa dhidi yake na baadhi ya
wajumbe wa baraza hilo; wengi wa wajumbe hawakubaliani wamekataa azma ya
mwenyekiti kutaka kujiuzulu na kuwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu
mdogo wa kisiasa na sawa na kuwa msaliti ndani ya UVCCM na iwapo
wangejua basi wangemchagua mgombea mwingine kata ya waliogombea .
Mwanahabari Tumaini Msowoya
alikuwa mwakilishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa kabla ya kuhamia
gazeti ya Uhuru na Mzalendo mkoa wa Iringa alipata kushinda kwa
kishindo kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) wa mkoa wa Iringa Oktoba, 2012.
Katika uchaguzi huo, jumla ya
kura 302 zilipigwa ambapo Msowoya alipata kura 188 akifuatiwa kwa mbali
na mwanahabari Abba Ngilangwa aliyepata kura 76 huku Ramadhani Baraza
akiambulia kura 36.
Alipopewa nafasi ya
kuwashukuru wajumbe kwa kumpatia ushindi huo, Msowoya alisema anafahamu
kazi ngumu aliyoanayo mbele yake ya kuwaangunisha vijana wa mkoa mzima
wa Iringa ili kukiletea ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa
2015.
“Uongozi unapimwa kwa mambo
mengi lakini unapokuwa katika siasa sifa kubwa ni kukisaidia chama chako
kupata ushindi,” alisema huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wadau
mbalimbali wakiwemo wanahabari.
Katibu wa UVCCM mkoa wa
Iringa Alawi Haidar ametibitisha kutangaza kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo
japo alisema hadi sasa hajapokea barua rasmi kwa mujibu wa kanuni za
UVCCM kutokana na kiongozi anapohitaji kujiuzulu ni lazima kuandika
barua
Post a Comment