Mke
wa Makamu wa Raisi Bi Asha Bilali akipata maelezo ya Kujiunga na Mfuko
wa hifadhi ya Jamii wa PPF Kutoka kwa Meneja Mahusiano na Masoko wa
Mfuko huo wa PPF Bi Lulu Mongere wakati alipofika katika banda la PPF
kwenye Tamsha la Wanawake na Akiba katika Ukumbi wa Dar Live mapema leo
Mgeni
rasmi wa tamasha la Wanawake na Akiba na ambae ni Mke wa Makamu wa Raisi
Tanzania Bi Asha Bilali akijaza fomu ya Kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii wa PPF wakati alipotembelea banda la PPF kwenye Tamasha la
wanawake na Akiba lililofanyika leo Katika Ukumbi wa Dar Live,
Wanaoshuhudia ni Maafisa wa Mfuko wa PPF.
Mgeni
rasmi ambae pia ni Mke wa Makamu wa raisi wa Tanzania Bi Asha Bilali
akipigwa picha kwaajili ya kupata kitambulisho cha PPF mara baada ya
kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa PPF mapema leo katika Tamasha la
Wanawake na Akiba lililofanyika katika Ukumbi wa Dar Live mapema leo,
Wanaoshuhudia pembeni ni Maafisa wa Mfuko wa PPF.
Mgeni
rasmi ambae pia ni Mke wa Makamu wa Raisi wa Tanzania, Bi Asha Bilali
akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa mfuko wa hifadhi ya Jamii wa
PPF wakati alipotembelea Banda la PPF leo katika tamasha la Wanawake na
Akiba lililofanyika katika Ukumbi wa Dar Live mapema leo asubuhi.
Meneja
Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF Bi Lulu Mongere
(Wa kwanza kulia) akitoa Maelezo Kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika
katika Banda lao Kwaajili ya Kujiunga na Mfuko wa Hiari kutoka PPF.
Mkazi
wa Jiji la Dar ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifurahia
kuchukua fomu ya kujiunga na Fao la Hiari kutoka Mfuko wa hifadhi ya
Jamii wa PPF mara baada ya kufika katika banda lao kwenye Tamasha la
Wanawake na Akiba lililofunguliwa leo Katika Ukumbi wa Dar
Live.Anayempatia Fomu ni Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii wa PPF Bi Lulu Mongere
Meneja
Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bi Lulu Mongere
akitoa maelekezo ya ujazaji wa fomu za kujiunga na Fao la Hiyari kwa
wakazi wa jiji la Dar Waliofika katika banda lao lililopo kwenye Tamasha
la Wanawake na Akiba lililofanyika Katika Ukumbi wa Dar Live.
Wakazi
wa Jiji la Dar Wakipata maelezo juu ya kujiunga na fao la hiyari kutoka
kwenye mfuko wa hifadhi wa jamii wa PPF kutoka kwa Maafisa wa Mfuko huo
wa PPF katika banda lao lililopo katika Tamasha la Wanawake na Akiba
lililofanyika leo katika Ukumbi wa Dar Live.
Wakazi
wa Jiji la Dar Wakifurahi pamoja na Maafisa wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Wa PPF mara baada ya Kujiunga na Mfuko huo wakati walipofika
katika Banda la PPF kwenye Tamasha la Wanawake na Akiba lililofanyika
katika Ukumbi wa Dar Live Mapema leo asubuhi.
Post a Comment