![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiciH_5yx-TX8cDk0rJHuYBAVNXmVQfdTHg_jQlOcxYVN_Y06FYhmXM8ok2OUsQSvG4LBKnM948HNIzKiUhfcG_NBYPY0aYdkr9xETu8gSHnF-72MlaFec-97TdtGe7ZDs4_uN3hSQC0T0/s1600/Sanaa.Still019.jpg)
Msanii
aliyetamba enzi hizo kwa umahili wake wa kuchea na nyoka Salma Moshi
akisalimiana na kumkabidhi picha za baadhi ya kazi ya sanaa hiyo
aliyofanya enzi hizo Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani Mhe. Liberata Mulamula alipokwenda kujitambulisha rasmi kwenye
Ubalozini wa Tanzania uliopo Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18,
2014.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghHdrOj0q7yXmHpzfDijTs54pqeRUmaIXGbp2tS1M4qswNL1prVXXnxz82RFQptrdIk3nbx78mXM9t685npSxCqgakcHQD7_Sl50cLO_hyphenhyphenQTgB10ITmeM66vWEdH691scG2nbzshsrL_o/s1600/Sanaa.Still021.jpg)
Msanii
wa siku nyingi na mahili wa kucheza na nyoka Bi. Salma Moshi aliongea
na Mhe. Balozi Libetara Mulamula alipotembelea Ubalozi wa Tanzania
Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_Zz2eBgFIdlVxKw7d7sbhIuNXBB9oXAd-GvUr3rIpTvplmHCPRAwJaHQUU5-UBppSkNL4qwE-50wWdVSOBil5bxqedKHvMeo1uTRFfH4jmbtvdsJx46uiqEEnf494pG9fVJeoIAPSy2g/s1600/Sanaa.Still010.jpg)
Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania nchini Marekani, Mhe. Liberata
Mulamula akimsikiliza msanii wa siku nyingi, Bi Salma Moshi (hayupo
pichani) alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya
Jumanne Feb 18, 2014.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjv9ih_5H0mKMWcPzpy21q_zyWEFqAEZtwoCKJP7ZzMxhFErBVGZ0kvJyU9-5__s1HDl-JXWOlitKQKW_8ka1Yt3i2CMfh5y0nRN8aCDuNcuJ630XXj8ijTKWLe3JHK1qVoVWZmHaYhAyo/s1600/Sanaa.Still005.jpg)
Afisa Mgendi Nzowa akiwa kwenye mkutano huo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZK_UTohtokN6GUk1fL0nzx2tub1UdF2qeplxtg0t_18_L-2mjPcdUiwoA2xWXk850mNsV9umpzd8tHH743lGk-qfXvlrGS-Mzy1H28pqk_rehQv-mLno5BsJT9jWil1rB2GcyZm88hhw/s1600/Sanaa.Still008.jpg)
Afisa Suleiman Saleh akijumuika pamoja na Balozi kwenye mkutano huo.
Wito
hou umetolewana msanii wa siku nyingi wa kucheza na nyoka Mama Salima
Moshi alipokwendakumuona MH Balozi Mama mulamula Balozi wa Tanzania
nchini Marekani mama Salima alisema Balozi zina nafasi nzuri za
kuutangaza utamaduni wetu kwani wapo karibu na nchi husika na hivyo
kuviwezesha vjkundi kuja kufanya maonyesho pia aliomba BARAZA LA SANAA
LA TAIFA kuandaa kitabu kitakachojumuisha wasanii mbalimbali na anwani
zao vitabu hivyo vipelekwe kwenye balozi zetu ili watu mbalimbali
wanaokuja waweze kuvisoma na hatimaye kuwaalika wasanii wataweza
kuutangaza utamaduni wetu na wasanii kujipatia kipato na pia kujifunza.
mama
Salima alisema MAPROMOTA wengi baada ya kupata wamekuwa wanawatelekeza
wasanii na pato kubwa linaenda kwao bili kunufaisha msanii na hata wale
wanaobahatika kuja kupiga nje wamekuwa wanaishia kuwapigia watanzania
ifike wakati wakija huku waweze kutumbuiza na wenyeji wa huku alitoa
mfano kama JZ aende Tanzania halafu awapigie waMEREKANI
mama
Salima alikemea vikali swala la kukopi kazi za sanaa linarudusha nyuma
maendeleo ya wasanii na aliomba SERIKALI kutoa adhabu kali kwa watakao
bainika na kusimamia swala la hakimiliki mama salima alisema imefika
wakati sasa wasanii kuwa na WANASHERIA hii itasaidia kulinda haki zao
Mama salima alimshuru sana MH RAIS amekuwa wakati wote karibu
na wasaniina hata hivi karibunialiwaalika kwenye chakula hivyo naomba
wasanii tuitumie nafasi hiyo
Alisema
kuhusu tunzo ziwe zinatoa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho na
wakati umefika kutoa kibali kwa waandaaji wengine si vibaya zikawa zaidi
ya moja pia aliombakusaidia kujenga maktaba kwenye eneo la viwanja
vya wasanii MKURANGA na kumpongeza mwenyekiti wa wasanii bw TWALIBU
MH
BALOZI alimshukuru sana msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya
kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine
alisema kuhusu Hakimiliki SERIKALI imejizatiti kikamilifu
kuhakikisha haki za msanii zinalindwa alisema ni vyema wasanii wakajua
haki zao hii itawasaidia sana aliongolea MAPROMOTA ni vyema kuangalia
maslahi ya wasaniikwanza MH Balozi alisifu sana kazi zinazofanywa na
wasanii mbalimbali nchinina kuitangaza NCHI yetu
Post a Comment