Baraza
la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti
ya sh.bilioni 121 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa
Yusuph Mwenda alisema fedha hizo zimetokana na makusanyo ya vyanzo
vya mapato , pesa kutoka ruzuku serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo
ya ndani ya Halmashauri .Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa kujiendesha
kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa ikijiendesha kwa
asilimia 20 tu.
Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo la kutekeleza mipango ya maendeleo
na kuwaondolea umaskini wakazi wa kinondoni na kuboresha maisha
yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni.



Post a Comment