Haya ni mapigano ya kwanza tangu kutia saini mkataba wa kusitisha vita
Mapigano
yanaripotiwa kuzuka Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu serikali na
waasi kutia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi Januari.
Waasi
wanaomtii makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, wameshambulia mji wa
Malakal, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile linalozalisha mafuta
kwa wingi.
Majeshi ya serikali, yamepambana vikali na waasi hao katika maeneo tofauti ya mji huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Juba, (Toby Lanzer), amezitaka pande zote kwenye mzozo huo, kulinda raia.
Makabiliano
hayo bila shaka yanazua wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika visima
vya mafuta Kaskazini mwa nchi. Mafuta ya Sudan Kusini ndio uti wa mgongo
wa uchumi wa nchi hiyo.Chanzo BBC Swahili


Post a Comment