Mbunge wa Jimbo
la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameanzisha vilabu 102 vya
michezo kwa kuvipatia jezi na mipira ili kuhakikisha vijana wa jimbo
hilo lililopo mkoani Lindi hawajishughulishi na matukio ya uhalifu .
Majaliwa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu TAMISEMI aliyasema
hayo hivi karibuni wakati wa kilele za sherehe za kutimiza miaka 37 ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika katika kata ya Likunja
wilayani humo.
Katika
sherehe hizo Mbunge huyo alizipatia timu za mpira wa miguu za Uhuru
City na Mbagala City jezi seti moja kwa kila timu na mpira mmoja ambapo
timu hizo zilipanda uwanjani na kuchuana yote hiyo ikiwa ni
kusherehekea CCM kutimiza miaka 37 .
Baada
ya kumalizika kwa mashindano hayo timu ya Uhuru City iliibuka mshindi
wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya timu ya Mbagala City.
Naibu
waziri Majaliwa pia ameviwezesha vikundi mbalimbali vya ngoma katika
wilaya hiyo ambavyo vinajipatia pesa kwa ajili ya kazi ya sanaa na
kuweza kujikwamua kiuchumi.
Sherehe
hizo zilienda sambamba na maandamano ya wanachama wa Chama cha
Mapinduzi na kupambwa na burudani ya ngoma za asili, kwaya na mziki
kutoka kwa wasanii mbalimbali kikiwemo kikundi cha Wanapakaya kutoka
wilayani Kilwa na msanii Dogo Doto.


Post a Comment