Mgombea
Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu
na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya
Stendi-kata ya Ifunda.
Mapokezi
Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea
Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa
Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni
za Ubunge Jimbo la Kalenga.
Mh:Naibu
Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la
Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya
Stendi Kata ya Ifunda.Chief
Wa Wahehe,Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi
akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey
William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu
Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya
Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni Mtoto wa Marehemu
Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono
Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia
muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu
damu,na ameapa atafia CCM.
Msanii
Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi
wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga
wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William
Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,
Katibu
Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha
baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili
Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapata matatizo.Pia Ndugu
Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua
zaidi za kisheria.
Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana
Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.
Wabunge
wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa
Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.
Ni
Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya
Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo
kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la
Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua
Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia
Wananchi wa Kelenga,Lakini pia ni Kijana aliyependekezwa na Chama
kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na
amewashinda wenzake 9.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa
namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima
Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM
iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu
kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia
kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake
hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo
la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya
Jimbo hilo.
Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na
Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee
kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa
na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili
hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza.
Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba
ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za Ustaarabu,Kampeni za
Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali
tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya
siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi
wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na
Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote
wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey
William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.
Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.
Naibu
Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge
Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni
Jimbo la kalenga.Uchaguzi unategemewa Kufanyika tar.16/03/2014.
Picha zote na Habari kwanza Blog
Post a Comment