Naibu
waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo kwa
Wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma hii leo alipokutana nao kwenye Mkutano
wa ndani kwenye Ukumbi wa High Class One akizungumza nao kuhusu
Maendeleo ya Biashara,Ulipaji wa kodi,Changamoto za Mpakani kwenye
Ulipaji kodi,matumizi ya Mashine za EFD kwenye makato ya TRA.
Sehemu
ya Mamia ya Wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano wa Naibu Waziri wa
Fedha Mh;Mwigulu Nchemba wa Kujadiliana na kuelezana namna ya Kuimarisha
Ukusanyaji wa mapato nchini.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo ameendelea na Ziara
yake ya kikazi ya Kukutana na Wafanyabiashara ndnai ya Mkoa wa Mbeya
baada ya Kufanya hivyo kwenye Mkoa wa Njombe na Ruvuma wiki iliyopita.
Hii leo
Mh:Mwigulu amezungumza na mamia ya wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma
kuhusu nafasi yao ya Kukuza Ukusanyaji wa mapato kwa kaucha kukwepa
kulipa kodi,Kuacha kupitisha bidhaa kimagendo kwenye mpaka wa Nchi ya
Tanzania na Zambia.Wafanyabiashara Wakitanzania wasio wazalendo wa
Kulipa kodi wamekuwa wakitumia mwanya wa Mpaka kuvuka kufanya biashara
Zambia na makazi yao yapo Tanzania kitu kinachopelekea ukusanyaji wa
Mapato kuwa Mgumu kwa TRA na taasisi husika. Serikali imeamua kufanya
maridhiano na Serikali ya Zambia kuhakikisha kunakuwepo na Mpaka
uliotenganishwa kwa Mita 50 kila upande wa Nchi hizi mbili ilikudhibiti
ukwepaji wa kulipa kodi na biashara ya Magendo.
Naibu
waziri pia alitumia nafasi kuwaelimisha Wafanyabiashara umuhimu wa
kutumia mashine za EFD kwenye kurahizisha ukusanyaji wa mapato na kukuza
biashara zao.Mbali na hayo wafanyabiashara walipata nafasi ya kutoa
mawazo,maoni yao kwa Naibu waziri wa Fedha namna ya Kuimarisha
Ukusanyaji wa mapato,Uelewa wao kuhusu Mashine za EFD na Ushirikiano
watakao onesha kwenye Kudhibiti ukusanyaji mapato mpakani Mwatanzania na
Zambia.
Picha na Habari Kwanza Blog


Post a Comment