Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano
wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga
mjini.
Wakazi
wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya
ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru
na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM.
Zakaria
Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia
wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na
kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na
ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
Sebastian
Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole
akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini
Shinyanga.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya
shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye
amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja
vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa
Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa
kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga
Mjini Ndugu Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi
zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga
mjni tarehe 26 Februari 2014.
Post a Comment