RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
--
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,
amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za serikali. Uteuzi
huo ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Walioteuliwa
ni Kibibi Mwinyi Hassan ambae anakuwa Ofisa Tawala wa wilaya ya Kusini Unguja,
kuchukua nafasi ya Abdulla Ali Kombo ambaye atapangiwa kazi nyengine.
Aidha,
amemteua Haji Machano Haji kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika
Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kuchukua nafasi ya Maulid Mussa Takrima
aliyestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Wengine
walioteuliwa ni Issa Ibrahim Mahmoud kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa
shughuli za serikali katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,
kuchukua nafasi ya Ahmad Kassim Haji ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Naibu
Katibu Mkuu katika ofisi hiyo.
Ameir
Makame Ussi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa
katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kuchukua nafasi ya Issa
Ibrahim Mahmoud ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali katika ofisi hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi
wa viongozi hao umeanza Febuari 25 mwaka huu.
Post a Comment