Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

REKODI MPYA YA MAPATO YA MANCHESTER UNITED HII HAPA ISOME

 
Screen Shot 2014-02-13 at 2.12.41 AM 
Manchester United imeripoti taarifa ya kuongezeka kwa mapato ya klabu hiyo kwa 11.6% kwa awamu ya pili ya mwaka wa kifedha wa klabu hiyo.
Mabingwa hao wa Barclays Premier League wamesema mapato yao yameongezeka kutokana ukuaji wa biashara yao ya matangazo na kuuza haki za matangazo ya TV ya kuonyesha mechi zao.
Mapato ya kuanzia kipindi cha October–December yamekuwa mpaka kufikia kiasi cha £122.9m ambapo matangazo ya kibiashara yaliongezeka kwa asilimia  18.8, wakati biashara ya kuuza haki za matangazo ya TV kwa ajili ya mechi zao yalipanda kwa asilimia 18.7

  Screen Shot 2014-02-13 at 2.16.38 AM

Jingine la kufahamu ni kwamba hii club ilifanikiwa kupata udhamini wa makumpuni sita ya kibiashara.
CEO wa klabu hiyo  Ed Woodward alisema kwenye taarifa rasmi:  ”Kwa mara nyingine tena tumeweka rekodi ya kuingiza mapato makubwa kutokana na mchango mkubwa tunaopata kutoka washirika wetu wa kibiashara, hali hii inakuja pamoja na kuwa hatufanyi vizuri sana uwanjani, ukiangali nafasi tunayoshika uwanjani, ni jambo la kusikitisha na kila mmoja wetu anajua hilo.”
Screen Shot 2014-02-13 at 2.16.15 AM
United kwa sasa wanashika nafasi ya 7 kwenye ligi na wanaweza kukosa nafasi ya kushiriki kwenye Champions League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.NA MILLARD AYO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top