Tangu
itoke taarifa ya Ray C kuwa sawa kiafya Watanzania wengi na mashabiki
wanatamani kumuona Ray C akiwa jukwaani ama wimbo wowote mpya toka
kwake,kama nawe hili lilikua swali lako hatimaye mwanadada Ray C kaamua
kulijibu.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram Ray C ameandika maneno haya ‘Naimiss steji
vibaya mno!!!!Likizo ya mwaka mzima Alhamdullilah!!!Mungu ni mwema
sana!!!Asante kwa afya baba yangu!!!Muda si mrefu narudi kazinina
uhakika mashabiki wangu wapenzi mmenimiss saba!kila kitu tayari
kimepikwa bado tu kuwaambia lini tu but nioombeeni heri wapenzi wangu
najua sana mmeimiss sauti ya Ray C All over the world!!!jinsi
ninavyowapenda na jinsi mlivyoniombea zawadi kama kumi hivi
nimewaandalia!!mtashaje sasa!!kama nawaona vile!!bila nyie hakuna Ray
C!!!Thank you so very much guys!!!my fans!my everything!!nawapenda
mno!!!
Mara
ya mwisho binafsi kumuona Ray C jukwaani ni kwenye Jukwaa la Serengeti
Fiesta 2013 pale Leaders ambapo alipanda kwenye jukwaa na Recho na kwa
pamoja waliperfoam wimbo wa Ray C.
Post a Comment