Na Mahmoud Ahmad
Serekali
imeweka nia kwenye suala zima la uwekezaji na hili linajidhihirisha
wazi kwenye maboresho ya sera na miundo ya sheria zinazohusu
uwekezaji,ongezeko la mitaji kutoka nje ya nchi pamoja na mageuzi ya
kiuchumi yanaosababisha kutengamaa kwa mfumo wa soko kwa kiwango
kikubwa.
Hayo yamesemwa na waziri wa kilimo chakula na ushirika inj. Christopher Chizza kwa niaba ya Mh. Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda wakati akifunga Kongamano la
uwekezaji kanda ya ziwa huku akitanabaisha kuwa serekali inaendelea na
juhudi za maksudi za kuweka taratibu mbambali kuleta mabadiliko chanya
katika sekta za uchumi.
Chiza
alisema kuwa katika siku za karibuni sera ya ubia kati ya serekali na
sekta binafsi na sheria zinazoitekeleza,inataka serekali na sekta
binafsi kutengeneza mahusiano yanaopelekaa mazingira chanya katika
ukuwaji wa uchumi wa nchi huku serekali ikiendelea kutoa vivutio kwenye
sera za kifedha na zisizo za kifedha kwenye sekta ya biashara ya nje.Pia
Tanzania imewekeana makubaliano treaties dhidi ya kodi inayojirudia
double taxation na nchi za Denmark,India,Italy
Norway,Sweden,Kenya,Uganda,Zambia na Finland huku ikiridhia mikataba
mbalimbali inayohusu haki na ukuaji wa uwekezaji nje ya nchi.Nae
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally RUfunga alisema kuwa alisema zipo fursa
nyingi zinazopatikana kwenye ukanda huu wa ziwa ambazo zinahitaji
uwekezaji katika ukuaji wa uchumi wa taifa hivyo majadiliano yetu haya
na wawekezaji yatoa fursa hizo kuweza kutupaiasha kiuchumi kwa wakazi
wa kanda yetu na Tanzania kwa ujumla.
Rufunga
alisema kuwa Kama sehemu ya juhudi za serekali ya kutoa nchi kutoka
kwenye kipato cha chini kwenda cha kati kuanzia mwa wa fedha 2013\14 kwa
kushirikiana na sekta binafsi na wabia wa maendeleo katika kutekeleza
mpango wa matokeo makubwa sasa hasa ndio lengo la kongamano hilo la
uwekezaji wa kanda ya ziwa.
Aidha
Rufunga aliwataka watendaji wa serekali kwenye ukanda huo kuanza
kubadilika na kuendana na kasi ya serekali katika kufanikiasha ukujai wa
uchumi na kuacha urasimu usio wa lazima.
Post a Comment