Na Gladness Mushi, Arusha
MAMLAKA
ya mapato TRA hapa nchini imetangaza vita kubwa kwa wafanyabiashara
wadogo na wakubwa ambao wanashinikiza mgomo wa kufunga biashara kwenye
maduka mbalimbali hapa nchini kwa visingizio vya kutotambua matumizi ya
mashine za kulipia kodi
Aidha
hatua hiyo inakuja wakati wafanyabiashara katika mikoa mbalimbali hapa
nchini kufunga maduka na kisha kushinikiza kwa wenzao wasitoe huduma kwa
ajili ya kupinga matumizi ya mashine hizo
Akitangaza
rasmi vita hiyo ambayo itafanyika katika mikoa yote hapa nchini kaimu
Kamishna mkuu wa mamlaka hiyo Rishedi Bade alisema kuwa serikali kamwe
haitaweza kuwafumbia macho wadanganyifu wa biashara ya aina yoyote ile
Alisema
kuwa kwa wafanyabiashara wa aina yoyote ile atakayekamatwa kuwa
anashinikiza mgomo basi wataweza kuchukuliwa sheria mbalimbali ambazo
zitawagarimu kwa kiwango kikubwa sana
Pia
aliwataka wafanyabiashara nao kutoingia kwenye mgomo ambao hauwahusu
kwani wanajitengenezea harasa zao wenyewe wakati wanaohitajika kutumia
mashine hizo za kielekroniki wamebainishwa kwenye sheri
“TRA
tunashangaa sana kuona kuwa wafanyabiashara wasiohusika wanafunga
biashara wakati wanaohusika ni wengine na kwa hali hiyo tunatangaa vita
sasa na wale ambao wanahamasisha mgomo”aliongeza Bade
Wakati
huo huo pia alisema kuwa watakaokamatwa wakiwa wanahasisha mgomo huo
hatua watakazochukuliwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani lakini pia
hata kuweza kuwafutia leseni zao za biashara
Katika
hatua nyingine alisema kuwa matumizi ya mashine hizo ni muhimu sana kwa
maendeleo ya taifa la Tanzania kwani zinaweka na kuanisha wazi juu ya
mapato halisi ya mfanyabiashara
Post a Comment