Mahmoud Ahmad Mwanza
Serekali
imetakiwa kukemea maovu na ufisadi ili wananchi wawe na imani na chama
chao na serekali iliyo madarakani kwani bila kukemea maovu yanayotokana
ubadhirifu wa mali za serekali kwa waliopewa dhamana kujali mifuko yao
badala yawalio wengi itazidi kukiumiza chama nakushindwa kukiamini kuwa
kinatetea wanyonge.
Akizungumza
kwenye kilele cha madhimisho hayo kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa
chama wa kata hiyo katibu wa CCM wa kata ya Mabatini Gerald Mashala
alisema kuwa kumekuwa na kawaida kwa watendaji wa serekali wasio
waminifu kufuja mali za umma na kwataka viongozi wa chama hicho
kuendelea kukemea maovu sanjari na ufisadi bila kmuonea haya yeyote
kwani sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza serekali
Mashala
pia aliwataka wakazi wa jiji la mwanza na Tanzania kwa ujumla kuacha
kutoa malalamiko pekee yake kwani hayasaidi katika ujenzi wa taifa na
badala yake wajitume kuliletea maendeleo taifa lao huu ndio uzalendo wa
kweli malalamiko pekee hayasaidi tunatakiwa kukemea kwa nguvu zetu zote
kila aina ya maovu na ufisadi.
”
Utaifa kwanza ndio silaha yetu katika kujikomboa kutokana na maovu na
ufisadi uliokithiti kwenye idara za serekali kwani malalamiko pekee
hayatatasaidia kuondokana na maovu na ufisadi hapa tupige vita kwa nguvu
zetu zote” alisisitiza Mashala.
Nae
mwenyekiti wa ccm wa kata hiyo Yasiry Fuad aliwataka watanzania kuwa na
mshikamano wakati huo tunapoelakea kwenye bunge la katiba nakuondoa
itikadi za kisiasa na kuvaa utaifa kwani katiba si ya kisiasa inahitaji
uzalendo wa hali ya juu katika kufikia mmustakabali wa taifa letu.
Post a Comment