Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Symbion Power Tanzania Limited
zimesaini makubaliano ambapo kampuni hiyo itasaidia kwenye maeneo matatu
ya mpira wa miguu wa vijana.
Makubaliano
hayo yametiwa saini leo (Februari 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF
jijini Dar es Salaam. Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesaini kwa niaba ya
shirikisho wakati upande wa Symbion aliyesaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Peter Gathercoles.
Maeneo
ambayo Symbion itasaidia ni ujenzi wa vituo viwili vya kuendeleza
vipaji vitakavyojengwa Kidongo Chekundu na Kinondoni mkoani Dar es
Salaam, mashindano ya Taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 12
(U12) yatakayofanyika mwaka huu na kuisaidia timu ya U17 ya Tanzania
(Serengeti Boys).
Serengeti
Boys itacheza na Afrika Kusini, Julai mwaka huu katika mechi za mchujo
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa wachezaji wa umri huo
zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Hivyo
Symbion imetoa dola 60,000 (zaidi ya sh. milioni 96) kwa ajili ya
mashindano ya U12, na dola 50,000 (zaidi ya sh. milioni 80) kwa ajili ya
maandalizi ya Serengeti Boys kwa mechi dhidi ya Afrika Kusini.
Rais
Malinzi ameishukuru Symbion kwa kukubali kushirikiana na TFF katika
mpira wa miguu wa vijana, lakini vilevile amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwani ndiye chachu ya kampuni hiyo
kuamua kujishirikisha na mpira wa miguu wa vijana.
Post a Comment