Mkurugenzi
wa Kampuni inayojihusisha na mafunzo ya ufundi ya European Erun ya
Nchini Uingereza Bwana Ramesh Kumar akizungumza na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wa Pili kutoka kulia waliokaa
kwenye ukumbi wa Msekwa ndani ya eneo la Bunge la Jamuhuri Mjini Dodoma.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo
na Mkurugenzi wa Kampuni inayojihusisha na mafunzo ya ufundi ya European
Erun ya Nchini Uingereza Bwana Ramesh Kumar mara baada ya mazungumzo
yao yaliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Msekwa Mjini Dodoma.
Kati kati yao ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban.
Mkurugenzi
wa Kampuni inayojihusisha na mafunzo ya ufundi ya European Erun ya
Nchini Uingereza Bwana Ramesh Kumar akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
Mkuu wa Shrika la Umeme Zanzibar { ZECCO } Nd. Hassan Ali Hassan Mjini
Dodoma.
Afisa
Miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Nd.Khalifa Muumin
akimpatia ufafanuzi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi juu ya ramani zilizokamilika kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za Mkopo
huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kushoto
ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar { ZSSF } Nd. Abdullwakil Haji Jecha mkutako uliofanyika nje ya
Makazi ya Balozi Seif Bara bara ya Farahani Mjini Dodoma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
******************************
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } unaendelea na utafiti wa namna ya
kutaka kuliimarisha eneo la kati la Mji wa Zanzibar ili liwe katika
hadhi inayokubalika Kimipango Miji sambamba na kuleta haiba nzuri ya
Mji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko huo Nd. Abdullwakil Haji Jecha alisema hayo wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
hapo nje ya makazi yake Bara bara ya Farahani Mjini Dodoma.
Nd.
Abdullwakil alisema Uongozi wa Mfuko huo umefikia uamuzi huo kufuatia
hatua nzuri iliyofikiwa ya ujenzi wa Kiwanja cha Kufurahishia Watoto cha
Uhuru –ZSSF kilichopo kariakoo na Mnara wa kumbu kumbu ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar miradi iliyo chini ya ujenzi wa Mfuko huo.
Alieleza
kuwa uimarishaji wa eneo hilo umelenga kujenga bara
bara zitakazokwenda sambamba na uwekaji wa mapembea ya kuchezea watoto
baina ya miradi hiyo miwili jirani.
“
Sisi tuko tayari na tumejiandaa kutumia wataalamu na washauri washirika
katika kuliimarisha eneo hilo kwa ujenzi wa mapembea Maduka ya Kisasa
kulingana na ushauri wa Taasisi inayosimamia mipango miji “. Alisisitiza
Nd. Abdullwakil.
Akizungumzia
ujenzi wa nyumba za mkopo zilizoko katika ramani ya ujenzi zinazotaka
kujengwa na Mfuko huo katika eneo la Mbweni Ndugu Abdullwakil Haji Jecha
alisema hatua za micho za michoro ya nyumba hizo imeshakamilika.
Aliiomba
Serikali Kuu kusaidia upatikanaji wa eneo maalum la uwekaji wa karakana
ya utengenezaji wa Matofali pamoja na vifaa vyengine vya
ujenzi litakalotumiwa na Kampuni iliyokubali kuingia ubia na Mfuko huo
ya Shumaka ya Nchini Marekani katiika ujenzi wa nyumba hizo.
Naye
Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban ambae alikuwepo kwenye mazungumzo hayo aliuahidi Uongozi wa
Mfuko huo kuupatia eneo la Buyu kwa ajili ya kuwekea kara kana yao.
Waziri
Shaaban alisema eneo hilo lilikuwa likitumiwa na Kampuni ya ujenzi ya
Engineering construction ambayo tayari imeshakamilisha mkataba wake hapa
Nchini.
Akitoa
Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliuagiza Uongozi huo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF }
kuwasiliana na mshirika wao wa ujenzi wa nyumba hizo za mkopo ili hatua
za mradi zianze mara moja.
Balozi
Seif aliutoa mashaka Uongozi wa Mfuko huo kwamba wateja wa ununuzi wa
nyumba hizo wapo wengi hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar hivi sasa
inaendelea kubadilika Kiuchumi na kibiashara Kiamataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Mfuko huo kwa
jitihada zake inazochukuwa za kuanzisha miradi tofauti yenye lengo la
kutunisha mfuko huo kwa faida na hatma njema ya wanachama wake.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni inayojihusisha na utoaji
wa mafunzo ya Ufundi { European Erum } kutoka London Uingereza.
Katika
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya muda ya Balozi Seif
iliyopo ndani ya jengo la Msekwa Bungeni Dodoma Mkurugenzi wa Kampuni
hiyo ya Europea Erum Bwana Ramesh Kumar alisema Taasisi yao imeonyesha
nia ya kutaka kujenga chuo cha ufundi Zanzibar.
Bwana
Ramesh ambae Kampuni yake tayari inefungua Matawi yake Ghana na Siera
Leon Afrika Magharibi alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umekusudia kuweka
Tawi lake Zanzibar ili kutoa huduma za Taaluma ya Kiufundi ndani ya
Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Alifahamisha
kwamba mradi huo utakaojumuisha Majengo la vifaa vyake Kamili umelenga
kutumia jumla ya Dola za Kimarekani Milioni tano ambazo ni kama mkopo
utakaorejesheka kutokana na ada za wanafunzi watakaojiunga na chuo
hicho.
Mkurugenzi
huyo wa European Erum alisisitiza kwamba taaluma itakayotolewa na
Kampuni hiyo ambapo wanafunzi wahusika waliomaliza Darama la Kumi na
Mbili na Kumi na Nne itamuwezesha mshiriki wa mafunzo hayo ya miaka
mitatu kuweza kujitegemea katika soko la ajira katika fani ya ufundi.
Naye
kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliuomba Uongozi wa Kampuni hiyo hiyo kuandika maombi maalum ya
uanzishwaji wa mradi huo wa uwekezaji utakaosaidia kwa kiasi kikubwa
suala la ajira kwa vijana watakaomaliza mafunzo yao.
Balozi
Seif aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada katika kuona mradi huo
unafanikiwa kuanzishwa hapa Nchini.
Mapema
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Ali Juma Shamhuna aliushauri
Uongozi huo kukifanyia utafiti chuo cha Ufundi Mbweni kama majengo yake
yanaweza kufaa kwa kuandishwa mradi huo.
Waziri
Shamuhuna alisema taaluma inayotolewa na Kampuni hiyo imeonyesha
kulingana na mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Ufundi Mbweni. Hivyo
utafiti huo unaweza kusadiai kupunguza gharama ya ujenzi wa majengo
mengine kwa ajili ya chuo hicho.
Post a Comment