Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA MAALUM YA IKULU KWA UMMA.




JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA



WIZARA YA FEDHA


TANGAZO KWA UMMA


            Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge.  Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha ongezeko hili.  Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.



               Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa Waziri alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio kweli bali ni maelezo binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo Serikalini wala Bungeni.



                             Aidha, tunapenda kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha Wabunge na Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana ukweli na uthibitisho wowote.

KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA


5 FEBRUARI, 2014
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top