Naibu
Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Naibu Kamishina
Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa Tanzania,Ndugu Patric
Kisaka(kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Ulipaji Kodi na Elimu
Ndugu,Richard Kayombo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Magreth
Kalenga(hayupo pichani) wakiondoka kwenye Ofisi za TRA Kuelekea kwenye
eneo la Mpakani Mwa-Tanzania na Mawali wilayani Kyela hii leo.
Kibao Kianachoonesha "KARIBU TANZANIA" kilichopo pembezoni mwa Mto Songwe unaotumiaka kama mpaka wa Tanzania na Malawi.
Huu
ndio Mto Songwe ambao ni Mpaka wa Tanzania na Malawi Wilayani Kyela.Huu
mto umeleelekea hadi Ziwa Nyasa na ndio Mpaka wa Tanzania na
Malawi,Lakini sehemu kubwa ya
Msafara
wa Naibu Waziri wa Fedha umefika kwenye hiki Kipenyo cha Mto
Songwe(Kinajulikana kama Timotheo) kinachotumika na Wananchi wasio
wazalendo Kuvusha bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania -Malawi au Malawi
kuja Tanzania.Ng'ambo ya Mto unaonekana ni mzigo mkubwa wa sukari
unaotarajiwa Kuvushwa kuja Tanzania kwa njia za Magendo na kubwa zaidi
Kukwepa Ulipaji Kodi.
Naibu
Waziri wa Fedha akiangalia Moja ya Mtumbi unaotumiaka kuvushia Biashara
za Magendo kwenye hiki kivuko haramu cha Timotheo kwenye Mto Songwe.
Naibu
Waziri na Msafara wake wakiwa kwenye Kivuko Kingine kisicho rasmi
kinachotumika Kuvushia bidhaa za magendo kutoka Nchi hizi mbili za
Tanzania na Malawi.Ng'ambo kwenye Nyumba zinazoonekana ni Nyumba za
Wananchi wa Malawi.Na kwa mbali kunaonekana roli likiwa limepakia Mzigo
unaodaiwa kuwa ni Mpunga uliovushwa kwa Magendo kutoka Tanzania kwenda
Malawi.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akifanya mahojiano na Vijana
waliokutwa wakivusha sukari kutoka Malawi kuja Tanzania.Vijana hao
wanadai wanalazimika kutumia njia hizi haramu kuvusha Sukari kutokana na
kuwa na mitaji midogo ya biashara zao,Hivyo kupita kwenye Kivuko Rasmi
cha Kasumulu wanakatwa Kodi Kubwa ambayo inawafanya wakose faida kwenye
Biashara yao.
Naibu
Waziri wa Fedha akizungumza na Watumishi/Watendaji wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Watumishi wa Idara mbalimbali zinazohusika na Mpaka wa
Tanzania na Malawi.
Na.Habari Kwanza Blog,
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu
Lameck Nchemba hii leo(Tar.04/02/2014) ameendelea na Ziara yake ya
Kikazi Mkoani Mbeya ya Kutembelea Vituo vya Ukusanyaji wa Mapato na
Kuangalia changamoto za Ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo ya Mipaka ya
Nchi.
Hii leo amefika Wilaya ya Kyela na
kukutana na Mkuu wa Wilaya Mh:Magreth Kalenga aliyeongoza kutembelea
maeneo ya Mpaka wa Tanzania na Mawali kutathimini namna Ukusanyaji wa
Mapato unavyokuwa na changamoto nyingi kutokana na Watanzania wengi
kukwepa Kulipa kodi kwenye Vivuko rasmi vya Mipaka.
Wilaya ya Kyela imetajwa kuwa na Vipenyo visivyo rasmi 32 vinavyotumika kupitisha bidhaa za magendo(sukari, Viroba,Mpunga n.k) ,Katika
hali ya kuonesha kuwa biashara ya Magendo imeshamili mpakani hapo,Naibu
Waziri wa Fedha ameshuhudia vijana wakivusha Sukari kutoka Malawi kuja
Tanzania kwenye kipenyo kisicho rasmi kinachojulikana kwa jina la
Timotheo.Katika mahojiano ya Mh;Mwigulu na Vijana hao,Watanznaia hao
wanasema walazimika kutumia njia hizo za panya kuvusha bidhaa hizo
kwasababu ya Ushuru kuwa Mkubwa na Mtaji wao ni mdogo,pia Ugumu wa
Maisha ndio unawafanya wakimbilie kutafuta faida ya haraka ilikusaidia
familia zao.
Naibu Waziri amesema Kupitia Wizara yake(Serikali) imejipanga kufanikisha haya.
1.Kuhakikisha upatikanaji wa
bidhaa(Sukari n.k) nchini unaongezeka ilikutoa nafasi ya
wafanyabiashara kuchana na biashara za magendo za kutumia bidhaa za
Malawi kwa njia ya kukwepa kodi.
2.Kuongeza Watumishi wa Kwenye Mipaka
wanaohusika na Usalama,Ukusanyaji wa Mapato n.k ilikuhakikisha huduma
zinatolewa kwa wakati bila usumbufu wowote.
3.Pia Ujenzi wa kituo kituo cha
Pamoja(One-Stop Border Post) cha Ukaguzi kati ya Nchi ya Tanzania na
Malawi ilikuondoa Urasimu na Ucheleweshwaji wa kupitisha bidhaa kwenye
vivuko vya Mipakani.Mazungumzo yameshaanza na Utekelezaji unategemea
kuanza mapema.
3.Kuongeza Upatikanaji wa Elimu kwa
Wafanyabiashara kuhusu athari za kukwepa kodi,faida za kutumia Vivuko
rasmi kwenye upitishaji wa bidhaa zao.


Post a Comment