ISO
9001: 2008 CERTIFIED
TAARIFA
KWA UMMA
Mamalaka ya Mapato Tanzania
inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wafanyabiashara kwa ujumla Kuwa
inasikitishwa na mgomo wa wafanyabishara
kwa kufunga maduka maeneo mbali mbali nchini.
Ifahamike kuwa Matumizi ya
mashine ya EFD ni jambo la kisheria na
lilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2011.
Pamoja na sheria kupitishwa,
viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko kwa nyakati tofauti kwa kuanzia
na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika
hotuba yake ya kufunga mwezi wa Machi 2011.
Pia Makamu wa Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Billal alikazia jambo hili
tarehe 8 Mwezi November mwaka 2013.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya
Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alilitolea tamko pia Mwezi Desemba
2013 wakati akiahirisha Bunge kwa
kusisitiza msimamo wa serikali kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi wa
mashine za EFD.
Tarehe 29 Janauri 2014,
Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya Salum aliweka bayana msimamo wa Serikali kwa
kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni swala la kisheria na litaendelea
kutekelezwa kwa mujibu wa sheria akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa nyongeza
kwa wafanyabishara kununua mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014 baada ya
kuongeza muda mara tatu kwa nyakati tofuati.
Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) pia kwa nyakati tofauti na maeneo tofuati imelitolea tamko jambo hili na
itaendelea kufanya hivyo.
Kwa masuala ya kiutendaji
yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo utoaji wa Elimu kwa
umma.
Mamlaka ya Mapato
Tanzania inapenda kuwafahamisha
wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa watu wanaolazimisha wafanyabishara
wenzao kufunga maduka kwa kuwatishia na kuwashurutisha wanavunja sheria kwa
kusababisha uvunjifu wa amani nchini na hivyo mkono wa sheria utawafikia. Pia
imefahamika kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa
bali hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya
TRA imekuwa ikipokea taarifa
na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara na wananchi wema wakiomba ulinzi
ili wafungue maduka yao na kufanya biashara maana ndio ajira yao na mahali
pakujipatia riziki ya kila siku.
Ifahamike kwamba wale wote
wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja sheria kwa kuwalazimishwa
wafanyabiashara kugomea agizo halali la kisheria hivyo kwa wale wote wanaotishiwa
au kushurutiswa watoe taarifa kwa kupiga
simu namba zifuatazo 0786 800 000, 0713 800333, 0800 110016 au barua pepe info@tra.go.tz
“PAMOJA
TUNAJENGA TAIFA LETU”
IMETOLEWA
NA KAIMU KAMISHNA MKUU
MAMLAKA
YA MAPATO TANZANIA
Post a Comment