Prof.
John Nkoma akitoa Maelezo KWA Mh. Waziri wa Fedha kabla ya kukabidhi
hundi ya Mapato ya Mtambo wa Mawasiliano wa TTMS. Katika tin I Waziri wa
Fedha Mh. Saada Mkuya, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Mama Mwanyika. Kulia ni Viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano
walioongozana na Prof. Nkoma, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bw.
Alinanuswe Kabungo, Mkurugenzi wa ICT wa TCRA Dr. Joseph Kilongola na
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha Bw. Wilfred Maro
Profesa
Nkoma akikabidhi cheki hiyo ya pili KWA Viongozi wa Wizara ya Fedha
alisema, TCRA KWA mujibu wa sheria hiyo, umekuwa ikitimiza wajibu wake
KWA serekali bila kuchelewa Na KWA mwaka huu wa fedha tayari TCRA
ilishatoa tena cheki yenye thamani kama hiyo kwa robo mwaka ya kwanza na
imebaki malipo ya robo ya tatu na ya nne KWA mwaka huu wa fedha.
Na Innocent Mungy
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, imetoa malipo ya kwanza ya mtambo wa TTMS
(mtambo Maalum wa usimamizi wa Mawasiliano ya Simu) kwa serekali
Kufuatia kukamilika Kwa mtambo huo na kuanza kufanya kazi tangu mwezi
Oktoba mwaka jana.
TCRA
iliwasilisha fedha hizo Hazina, Kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, tukio
hilo likishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya.
Akizungumza
katika ghafla ya kukabidhi hundi ya kwanza ya mapato hayo kwa Serekali,
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John S. Nkoma alimweleza Mh. Waziri wa
fedha kuwa, TCRA imekamilisha kuujenga mtambo huo na umeanza kufanya
Kazi tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2013. Cheki hiyo ni mapato ya mwezi
huo wa Oktoba ambapo kiasi cha shilingi 1,688,299,014.40 zimelipwa kwa
serekali kufuatia maelekezo ya Kanuni za TTMC kuwa serekali inapata 28%
ya mapato ya simu zinazopigwa kutoka nje ambayo ni cent 7 ya dola kwa
dakika.
Mgao wa
mapato ya mtambo huo uliojengwa TCRA KWA mfumo wa BOT (Build, Operate
and Transfer) umefanikiwa kuongeza pato la serekali baada ya wataalamu
wanashiriki ana na TCRA katika mradi huu kufanikiwa kupata cent 25 ya
dola KWA dakika toka kwa makampuni ya nje yanayotumika kupiga simu
Tanzania, awali Tanzania ikipata cent 8 tu ya dola KWA dakika.
KWA
mujibu wa Kanuni hizo, Makampuni ya Simu hupata 52% ya mapato (senti 13
kati ya25) Serekali 28% (senti 7 ya dola katika 25) na Mwekezaji katika
mradi huo SGS ya Uswiss hupata asilimia 20%(senti 5 ya dola kati ya 25).
Akizungumza
katika ghafla hiyo, Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya aliipongeza TCRA
KWA kufanikisha mradi huo na kutoa gawio la kwanza KWA serekali KWA
uaminifu. Aidha alisema mradi huo utakaoongeza mapato ya serekali, uende
she vizuri ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo KWA wafanyakazi wanafanya
Kazi katika kitengo cha TTMS ili kuwa na weledi zaidi.
Aidha
Prof. John Nkoma alimkabidhi Mheshimiwa Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara ya fedha cheki ingine ya shilingi 1,625,000,000 (shilingi bilioni
moja na milioni Mia Sita) kama sehemu ya maagizo ya Sheria ya Fedha ya
Mwaka 2008 inavyoelekeza kuwa Taasisi za Serekali zinazokusanya mapato
kutoa asilimia 10% ya mapato ghafi ya makusanyo yake kwa serekali.
Post a Comment