Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki wakati
alipotembelea Banda la Kituo hicho kwenye Maonyesho ya Kongamano la
Uwekezaji yaliyoanza jana kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza
.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo ambaye ndie
Mwenyeji wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (katikati)
akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya
Kanda ya Ziwa ,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey
Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya
Ziwa,Mh. George Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akibadilishana Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki mara
baada ya kusainiana na wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,jijini Mwanza
jana.Shughuli hii imefanyika wakati wa Muendelezo wa Kongamano la
Uwekezaji Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki
akizungumza wakati alipokutana na baadhi ya wawekezaji wenye leseni za
TIC (hawapo picnani) ,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Jijini
Mwanza jana.
Mmoja wa Wawekezaji waliopo ndani ya Kanda ya Ziwa,akiwasilisha jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki. Picha Zote na Othman Michuzi, Mwanza.
Post a Comment