JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA
MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
UZIMAJI MITAMBO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA AWAMU YA
PILI
1.0 UTANGULIZI
Mamlakaya
Mawasiliano imepokea matokeo ya tathmini ya zoezi la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijitAali.
Zoezi hili lilifanyika kwenye miji saba kama ilivyotajwa kwenye taarifa iliyotolewa na wataalamu wa
Chuo kikuu cha Dar e salaam waliofanya tathmini ya Uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya
Kwanza.
Mamlakaya
Mawasiliano
Tanzania (TCRA) ilifanya kamisheni kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
kufanya tathmini ya uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya
Kwanza, ikitambua kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuna wataalamu wenye
uzoefu mkubwa wa kufanya tathmini za aina mbalimbali, na kwamba uzoefu
huo utasaidia sana kuhakikisha kuwa tunapata taarifa ya uhakika
itakayotuwezesha kuboresha zoezi hili kwenye awamu inayofuata.
Nachukua
nafasi hii kuwapongeza wataalamu waliohusika katika tathmini hii kwa
weledi wao kwenye kazi hii muhimu kwa taifa letu kulingana na matokeo
yaliyowasilishwa kitaalamu mbele yenu waandishi wahabari leo hii.
Tanzania
ninchiya
kwanza kuzima mitambo ya analojia Barani Afrika. Uamuzi wa kufanya
hivyo,
na matokeo yake, umeiletea sifa kubwa nchi yetu kwa jinsi ambavyo
Tanzania ilijipanga na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kimataifa
kwa wakati na weledi mkubwa.
Hii
imeonyesha wazi jinsi Serikali ilivyo weza kushirikiana na taasisi zake
pamoja na wadau wote katika kutimiza azma hii iliyoafikiwa kimataifa
tangu
2006.
Zoezi
la uzimaji mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza taree 31 disemba 2013 haikuwa rahisi kama wengi wetu tunavyoweza kufikiria,
kwani liligusa nyanja nyingi zikiwemo za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa.
Mamlaka
kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano, ilibidi kuzingatia matakwa ya
nyanja zote na wadau mbalimbali bila kuathiri utoaji wa habari nchini.
Inakadiriwa kuwa mpaka kumaliza zoezi hili, mitambo ya kurushia matangazo kwa mfumo wa analojia isiyopungua
60 itakuwa imezimwa.
Hali hii imefanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na kuifanya nchi yetu kuwa kituo
cha mafunzo kwa nchi nyingi ambazo sasa zimeku wazi kufika kujifunza hapa nchini.
Uamuzi wa kufanya mkutano wa nchiza SADC na ule
wa nchi za Jumuiya ya Madola kuhusu Mfumo mpya wa utangazaji wa kidijitali kwa sekta
ya utangazaji hapa nchini hivi karibuni, matokeo ya mafanikio makubwa tuliyoyapata
kwenye zoezi hili lililoendeshwa kitaalamu na Serekali yetu kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
1.0
UPELEKAJI WA MKONGO WA
TAIFA KWENYE VITUO VYA KURUSHIA MATANGAZO.
Mamlaka ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Wizara
na Kampuni ya Simu ya TTCL tuko kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa vituo vyote
vya kurushia matangazo vinafikiwa na mkongo waTaifa (Optic fiber cable). KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Madhumuni ya jitihada hizi, nikuona kuwa mbali
na huduma ya msingi ya kurusha matangazo ya televisheni, vituo vya utangazaji vinatoa
huduma za ziada zipatikanazo kwenye mfumo wa kidijiti.
Kwa lugha ya kitaalamu ni “interactive
services”.
Napenda kuchukua nafasi hii kuvitaka vituo vya utangazaji vyote
nchi ni kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizopo kwenye teknolojia hii ya kidijiti
ili wananchi waweze kuona tofauti kubwa kati ya mfumo wa zamani wa analojia na huu
mpya wa kidijiti.
3.0 UZIMAJI MITAMBO YA
ANALOJIA AWAMU YA PILI
Baada ya kupokea matokeo ya tathmini Awamu ya
Kwanza, Mamlaka ya Mawasiliano inajipanga kuzima mitambo kwa awamu ya pili na ya
mwisho.
Katika awamu hii, inategemewa miji 12
itahusika na uzimaji wa mitambo ya analoja.
Lakini kama maafikiano yalivyofanyika awali,
uzimaji utafanyika tu pale ambapo huduma za utangazaji wa kidijiti umefika.
Vigezovyotevitanotulivyokubaliananawadauvitahakikishwakuwavinatimizwakablayakuzimamitambohiyo.
Ni matarajio ya Mamlaka kuwa wasimikaji wa mitambo
ya kidijiti (Multiplex Operators)
wataendelea kwa kasi ufungaji wa mitambo hiyo hasa kwenye maeneo ambayo mfumo wa
analojia unatumika.
Mpaka sasa miji mingine 7 inapata huduma ya matangazo
ya kidijiti nayo ni Morogoro, Singida, Tabora, Musoma, Kigoma, Bukoba na Kahama.
Mchakato wa kufunga mitambo ya kidijiti kwenye
miji iliyobaki inaendelea vizuri.
Tunatarajia kuwa vituo vya utangazaji vitatoa ushirikiano
mkubwa kama ule tulioupata kwenye awamu ya kwanza.
Mamlaka imeyachukua mapendekezo yote yaliyotolewa
kwenye ripoti hii na tunaahidi kuwa tutayafanyia kazi. Yale yaliyo nje ya uwezo
wetu tutayafikisha mahali panapohusika kwa utekelezaji zaidi.
''Napenda kuwafahamisha kuwa Mamlaka
imependekeza rasimu ya ratiba ya uzimaji mitambo awamu ya pili na ya mwisho itakayotangazwa
na Waziri mwenye dhamana ya sekta ya Mawasiliano hivi karibuni.
Katika mapendekezo ya Mamlaka, tunakusudia kuanza
awamu ya pili katika miji ya Singida na Tabora mnamo mwishoni mwa mwezi Machi
2014.
Miji mingine
katika awamu ya pili itakuwa Musoma, Bukoba, Morogoro, Kahama, Iringa, Songea na
Lindi. Awamu ya pili inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2014.
Nia ya Mamlaka ni kuona zoezi hili la uhamaji kutoka
mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa kidijiti linakamilika katika nchi
yetu kabla ya kufikia ukomo wa matangazo ya analojia kama ilivyoelekezwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU) siku ya tarehe 17
Juni 2015''. alisema
Imetolewana:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO
TANZANIA
19 February 2014
Post a Comment