Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATAALAMU CHUO KIKUU WATOA RIPOTI YA UZIMAJI WA MITAMBO YA ANALOJIA

 


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZIMAJI MITAMBO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA AWAMU YA PILI
1.0  UTANGULIZI
Mamlakaya Mawasiliano imepokea matokeo ya tathmini ya zoezi la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijitAali.

 Zoezi hili lilifanyika kwenye miji saba kama ilivyotajwa kwenye taarifa iliyotolewa na wataalamu wa Chuo kikuu cha Dar e salaam waliofanya tathmini ya Uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya Kwanza.

Mamlakaya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya kamisheni kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufanya tathmini ya uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya Kwanza, ikitambua kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuna wataalamu wenye uzoefu mkubwa wa kufanya tathmini za aina mbalimbali, na kwamba uzoefu huo utasaidia sana kuhakikisha kuwa tunapata taarifa ya uhakika itakayotuwezesha kuboresha zoezi hili kwenye awamu inayofuata.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza wataalamu waliohusika katika tathmini hii kwa weledi wao kwenye kazi hii muhimu kwa taifa letu kulingana na matokeo yaliyowasilishwa kitaalamu mbele yenu waandishi wahabari leo hii.
Tanzania ninchiya kwanza kuzima mitambo ya analojia Barani Afrika. Uamuzi wa kufanya hivyo, na matokeo yake, umeiletea sifa kubwa nchi yetu kwa jinsi ambavyo Tanzania ilijipanga na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kimataifa kwa wakati na weledi mkubwa. 

Hii imeonyesha wazi jinsi Serikali ilivyo weza kushirikiana na taasisi zake pamoja na wadau wote katika kutimiza azma hii iliyoafikiwa kimataifa tangu 2006.
Zoezi la uzimaji mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza taree 31 disemba 2013 haikuwa rahisi kama wengi wetu tunavyoweza kufikiria, kwani liligusa nyanja nyingi zikiwemo za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa. 

Mamlaka kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano, ilibidi kuzingatia matakwa ya nyanja zote na wadau mbalimbali bila kuathiri utoaji wa habari nchini. 

Inakadiriwa kuwa mpaka kumaliza zoezi hili, mitambo ya kurushia matangazo kwa mfumo wa analojia isiyopungua 60 itakuwa  imezimwa. 

Hali hii imefanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na kuifanya nchi yetu kuwa kituo cha mafunzo kwa nchi nyingi ambazo sasa zimeku wazi kufika kujifunza hapa nchini.
Uamuzi wa kufanya mkutano wa nchiza SADC na ule wa nchi za Jumuiya ya Madola kuhusu Mfumo mpya wa utangazaji wa kidijitali kwa sekta ya utangazaji hapa nchini hivi karibuni, matokeo ya mafanikio makubwa tuliyoyapata kwenye zoezi hili lililoendeshwa kitaalamu na Serekali yetu kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
1.0          UPELEKAJI WA MKONGO WA TAIFA KWENYE VITUO VYA KURUSHIA MATANGAZO.
Mamlaka ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Wizara na Kampuni ya Simu ya TTCL tuko kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa vituo vyote vya kurushia matangazo vinafikiwa na mkongo waTaifa (Optic fiber cable). KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Madhumuni ya jitihada hizi, nikuona kuwa mbali na huduma ya msingi ya kurusha matangazo ya televisheni, vituo vya utangazaji vinatoa huduma za ziada zipatikanazo kwenye mfumo wa kidijiti.
Kwa lugha ya kitaalamu ni “interactive services”.
Napenda kuchukua  nafasi hii kuvitaka vituo vya utangazaji vyote nchi ni kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizopo kwenye teknolojia hii ya kidijiti ili wananchi waweze kuona tofauti kubwa kati ya mfumo wa zamani wa analojia na huu mpya wa kidijiti.
3.0   UZIMAJI MITAMBO YA ANALOJIA AWAMU YA PILI
Baada ya kupokea matokeo ya tathmini Awamu ya Kwanza, Mamlaka ya Mawasiliano inajipanga kuzima mitambo kwa awamu ya pili na ya mwisho.
Katika awamu hii, inategemewa miji 12 itahusika na uzimaji wa mitambo ya analoja.
Lakini kama maafikiano yalivyofanyika awali, uzimaji utafanyika tu pale ambapo huduma za utangazaji wa kidijiti umefika. 
Vigezovyotevitanotulivyokubaliananawadauvitahakikishwakuwavinatimizwakablayakuzimamitambohiyo.
Ni matarajio ya Mamlaka kuwa wasimikaji wa mitambo ya kidijiti  (Multiplex Operators) wataendelea kwa kasi ufungaji wa mitambo hiyo hasa kwenye maeneo ambayo mfumo wa analojia unatumika.
Mpaka sasa miji mingine 7 inapata huduma ya matangazo ya kidijiti nayo ni Morogoro, Singida, Tabora, Musoma, Kigoma, Bukoba na Kahama.
Mchakato wa kufunga mitambo ya kidijiti kwenye miji iliyobaki inaendelea vizuri.
 Tunatarajia kuwa vituo vya utangazaji vitatoa ushirikiano mkubwa kama ule tulioupata kwenye awamu ya kwanza.
Mamlaka imeyachukua mapendekezo yote yaliyotolewa kwenye ripoti hii na tunaahidi kuwa tutayafanyia kazi. Yale yaliyo nje ya uwezo wetu tutayafikisha mahali panapohusika kwa utekelezaji zaidi.

''Napenda kuwafahamisha kuwa Mamlaka imependekeza rasimu ya ratiba ya uzimaji mitambo awamu ya pili na ya mwisho itakayotangazwa na Waziri mwenye dhamana ya sekta ya Mawasiliano hivi karibuni.
Katika mapendekezo ya Mamlaka, tunakusudia kuanza awamu ya pili katika miji ya Singida na Tabora mnamo mwishoni mwa mwezi Machi 2014.
 Miji mingine katika awamu ya pili itakuwa Musoma, Bukoba, Morogoro, Kahama, Iringa, Songea na Lindi. Awamu ya pili inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2014.
Nia ya Mamlaka ni kuona zoezi hili la uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa kidijiti linakamilika katika nchi yetu kabla ya kufikia ukomo wa matangazo ya analojia kama ilivyoelekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU) siku ya tarehe 17 Juni 2015''. alisema
Imetolewana:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

19 February 2014
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top