Mbunge
wa jimbo la Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akimpa matibabu mchezaji wa
Shule ya Sekondari Kawe Thomas Ibrahim aliyeumia wakati wa mechi ya
ufunguzi wa mashindano ya Dar es Salaam Community Cup leoo katika
viwanja vya shule ya msingi Turiani.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Henry Lihaya
akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara(wa pili kushoto waliokaa0 wakati wa uzinduzi wa ligi
ya Dar es Salaam Community Cup leo katika viwanja vya shule ya msingi
Turiana Magomeni jijini Dar es Salaam. Ligi hiyo inashirikisha timu 12
kutoka shule za Sekondari za jiji la Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akizungumza na washiriki wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo
kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam wakati
akizindua rasmi mashindano hayo, kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga
penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa miguu
yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es
Salaam , aliyeko gorini ni ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Salum Mwalim.
Mchezaji wa Shule ya Sekondari Turiani akidhibiti mpira wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Picha zote na Frank Shija – Wizara ya Habari
Post a Comment