Marehemu AL Hajj Kabbah |
Amefariki nyumbani kwake akiwa na miaka 82.Alhaji Ahmad
Tejan Kabbah alizaliwa February 16, 1932. Aliongoza Sierra Leone kati ya mwaka
wa 1996 hadi 1997 na kisha tena mwaka wa 98 hadi mwaka wa 2007Katika miaka mingi ya utu uzima wake, alihudumu kama
mtaalamu wa uchumi na sheria. Alifanya kazi kwa miaka mingi na shirika la
maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP. Baada ya kujiuzulu kutoka umoja huo mwaka
wa 92, alirudi zake nchini Sierra Leone na kujiingiza katika siasa za nchi
hiyo
Maisha yake ya siasaMnamo mwaka wa tisini na sita, bwana
Kabbah alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama Sierra Leone's People's Party (SLPP)
na kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho mwaka wa 96.
Katika kinyanganyiro hicho, alishinda na kuwa rais kwa 59%
ya kura na kumpiku mpinzani wake mkuu John Karefa-Smart wa chama cha United
National People's Party (UNPP) aliyepata 40% tu ya kura.
Kikubwa atakachokumbukwa nacho ni hotuba yake ya kuapishwa
mjini Freetown, alipoahidi kumaliza kabisa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe,
jambo alilotekeleza baada ya kuwa rais.
Bwana Kabbah ni wa kabila la Mandingo kiasilia na ndiye
aliyekuwa rais wa kwanza wa kiislamu wa Sierra Leone. Alizaliwa katika kijijji
cha Pendembu, wilaya ya Kailahun mashariki mwa Sierra Leone, japo udogoni mwake
alikulia mji mkuu wa Free town.
Utawala wa KabbahSehemu kubwa ya uongozi wa Kabbah
ilishawishiwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyotokea nchini Sierra
Leone kwa muda mrefu, huku akikumbwa na mapinduzi ya muda yaliyofanywa na
wanamgambo wa United Front wakiongozwa na Foday Sankoh. Mapinduzi hayo
yalim'ngoa madarakani kati ya Mei 97 hadi March 98.
Post a Comment