Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajiwa kuhutubia bunge Maalum la KATIBA Kati ya Jumatatu na Jumanne
wiki ijayo.
Mwenyekiti wa bunge Maalum la KATIBA
Mheshimiwa Samuel Sitta ameliambia bunge Mara baada ya kuapishwa na
kukabidhiwa kiti chake leo jioni.
Amesema kazi ya kuwaapisha wabunge wote iliyoanza leo jioni itakuwa ikifanyika hadi saa 3 usiku na kukamilika Jumapili.
Jumatatu
wiki ijayo saa 10 jioni bunge hilo litakabidhiwa rasmi rasimu ya katiba
na mwenyekiti wa bunge la Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba.
Mwenyekiti
Sitta amemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa bunge
Hilo Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho kwa ustahimilivu, busara, hekima NA
uvumilivu aliouonyesha wakati akiliongoza bunge hilo kuandaa kanuni zake
kwa kipindi cha wiki Tatu.
Amesema
kazi ya kuandaa kanuni ilifanywa bila kanuni hivyo baadhi ya wabunge
walitumia fursa hiyo kufanya vitendo visivyokubalika.
Amewakumbusha
wabunge kuwa kanuni zimepatikana NA hivyo wazifuate vinginevyo wasije
wakamlaumu pale atakapochukua hatua kwa ukiukwaji aw kanuni hizo.
Akiwaaga
wabunge aw bunge Hilo, Mheshimiwa Kificho amewaasa wabunge aw bunge Hilo
kuwa na hekima, busara, subira NA hoja zenye mashiko wakati wakifanya
kazi hiyo NA kuangalia zaidi maslahi ya taifa ili kuwapatia wananchi
KATIBA ambayo haitawagawa bali itakayoimarisha umoja NA mshikamano wao.
Mheshimiwa Sitta na Makamu wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wameapishwa leo jioni na Katibu wa Bunge la Katiba
Bw. Yahya Khamis Hamad aliyekuwa na Naibu wake Bw. Thomas Kashililla.
Imetolewa na
Idara ya Habari MAELEZO, Dodoma,
Machi 14,2014.

Post a Comment