Mgeni
rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa (katikati)
akiwasili kufungua rasmi mafunzo ya siku nne juu ya sheria za kimataifa
za kazi kwa majaji na wasajili wa mahakama nchini yalioandaliwa na
Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika
la Kimataifa la kazi duniani kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na
Uganda, Alexio Musindo.
***********************************************
Na Damas Makangale, Bagamoyo
JAJI
wa Mahakama ya Rufani, Tanzania, Edward Rutakangwa amesema bado kuna
upungufu mkubwa wa majaji katika mahakama za Tanzania kiasi cha
kusababisha mrundikano wa kesi katika mahakama hapa nchini. MOblog
inaripoti.
Akifungua
rasmi mafunzo ya siku nne kwa majaji, wasajili na wasajili wasaidizi wa
Mahakama ya Kazi, Jaji Rutakangwa amesema kwamba pamoja na Mheshimiwa
wa Rais kuteua majaji bado kuna upungufu mkubwa wa majaji nchini.
“Tatizo
la majaji kuwa wachache ni la muda mrefu pamoja na juhudi za Mheshimiwa
rais kupunguza ukubwa wa tatizo kwa minajili ya kuleta ufanisi katika
idara ya mahakama,” amesema Jaji Rutakangwa
Amesema
mafunzo hayo ya siku nne yataleta matokeo mazuri kwa majaji na wasajili
wa mahakama katika kuleta haki kwa wafanyakazi na kufanya kazi kwa
viwango vya kimataifa vya kazi duniani.
Meza kuu ikipitia makabrasha yao kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo.
Jaji
Rutakangwa alilisisitiza kwamba kuna umuhimu wa majaji kujua haki na
sheria za kazi kwa hiyo mafunzo hayo yatatoa fursa kwao kuelewa sheria
za kazi ili kuwawezesha kutoa hukumu kwa kuzingatia sheria na haki za
wafanyakazi nchini.
Amesema
kuna umuhimu wa majaji na wasajili wa mahakama kuelewa kwa kina sheria
za kimataifa za kazi na jinsi ya kuzitumia katika mahakama za ndani ya
nchini.
Kwa
upande, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi Duniani, Kenya,
Tanzania, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo amesema Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa
walifanya mabadiliko kadhaa ya kijamii na kiuchumi.
Mmoja wa wawezeshaji kutoka Ghana akijitambulisha kwa washiriki wa mafunzi hayo.
Amesema
moja ya mipango ya serikali hizo mbili ni kuweka mazingira mazuri kwa
ajili ya soko huria pamoja na kuweka vyombo vya kudhibiti soko hilo kama
vile Mahakama ya kazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
“Shirika
la kazi duniani litaendelea kufanya kazi kwa karibu na mahakama ya kazi
pamoja na Tume Usuluhishi katika kuleta ufanisi katika sekta ya kazi
kwa kujali maslahi ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi duniani,”
amesema Musindo.
Jaji
wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa akifungua rasmi mafunzo ya
siku nne juu ya sheria za kimataifa za kazi kwa majaji na wasajili wa
mahakama nchini yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo.
Musindo
amesema katika mafunzo hayo yatatoa fursa kwa majaji na wasajili wa
Mahakama kujifunza sheria za kimataifa za kazi na utatuzi wa migogoro
katika sehemu za kazi.
Naye
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mgaya
amesema kwa kuwa sheria ya kazi ni mpya ya mwaka 2004 bado kuna majaji
na wasajili wa mahakama haifahamu vya kutosha ili kukidhi haya ya jamii.
Amesema
mafunzo hayo ya siku nne ni fursa pekee kwa majaji na wasajili wa
mahakama kujifunza sheria za kimataifa za kazi ili kuleta tija katika
maamuzi yao mbalimbali.
Baadhi
ya majaji na wasajili wa mahakama nchini wanaohudhuria mafunzo ya siku
nne juu ya sheria za kimataifa za kazi yalioandaliwa na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) mjini Bagamoyo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania,
Kenya, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo akizungumza na washiriki kwenye
mafunzo hayo mjini Bagamoyo.
Jaji
Regina Rweyemamu kutoka Mahakama ya kazi, akizungumza changamoto
mbalimbali wanazokutana nazo kama majaji katika mahakama za kazi nchini.
Baadhi
ya majaji na wasajili wa mahakama nchini wakifuatilia yanayojiri kwenye
ufunguzi wa mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) yanayoendelea mjini Bagamoyo.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw. Nicholas Mgaya
akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya siku nne kuhusu changamoto
katika mahakama za kazi, upungufu wa majaji na vitendea kazi kama moja
ya vitu vinavyochangia mrundikano wa kesi katika mahakama hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waajiri (ATE) Wakili, Cornelius Kariwa akitoa hotuba yake
kwa niba ya chama cha waajiri nchini umuhimu wa kufahamu sheria za
kimataifa za kazi duniani.
Baadhi ya wasijili wa Mahakama ya kazi wakiwa kwenye mafunzo ya siku nne yanayoendelea mjini Bagamoyo.
Mgeni
rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa (katikati)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi
duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Bw.
Alexio Musindo wakati wakielekea kupiga picha ya pamoja. Kulia ni Afisa
Mipango mwandamizi wa shirika la kazi duniani (ILO) Anthony
Rutabanzibwa.
Mgeni
Rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa akiwa katika picha
ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo ya siku nne yanayoendelea mjini
Bagamoyo.
Post a Comment