Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa sambamba na Mwakilishi wa Hoteli ya Waride Resort Bwana Massliano Bramucci
wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Huduma za akina Mama
wajawazito katika Kijiji cha Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mashine ya Uchunguzi wa maradhi mbali mbali ya Tumbao 'Utra
Sound' iliyomo ndani ya Kituo cha huduma za akina Mama wajawazito
kilichopoPwani Mchangani kilichojengwa kwa ufadhili wa 283 ni:-Hoteli ya
Waride Resort.
Ushirikiano
unaoendelea kuonekana Kwenye miradi kadhaa ya maendeleo inayofanywa kwa
pamoja kati ya wananchi na wawekezaji ni miongoni mwa mapenzi yaliyopo
baina ya pande hizo mbili zikilenga zaidi katika kuimarisha uchumi na
ustawi wa Jamii.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo mara
baada ya kukifunguwa Kituo cha Huduma za Wajawazito kilichopo pacha na
Kituo cha Afya Cha Pwani Mchangani Wilaya ya Kaskazini “A”, Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Kituo
hicho cha huduma za wajawazito kikiwa ni vifaa vyote muhimu vya akina
mama wajawazito kimejengwa kwa ufadhili wa Muwekezaji wa Hoteli ya
Waride Resort kwa gharama ya shilingi Milioni 500,000,000/- wakati kile
ya Afya ambacho tayari kimeanza kutoa huduma kimepata ufadhili wa
Muwekezaji wa Ocean Paradise zote za Pwani Mchangani kwa gharama ya
Shilingi Milioni 400,000,000/-.
Balozi
Seif alisema wakati wafadhili na wawekezaji tayari wameshaonyesha
muelekeo hamu kubwa ya kusaidia maendeleo ya wananchi wa maeneo
wanayoekeza Wananchi wenyewe wana wajibu wa kuitunza miradi hiyo ili
iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.
Alisema
hatua hiyo itasaidia kuwapa nguvu zaidi wawekezaji hao kuendelea
kusaidia kuunga mkono harakati za wananchi hao katika kujiletea
maendeleo yao pamoja na kustawisha maisha yao ya kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Hoteli ya
Waride Resort na ule wa Ocean Paradise kupitia muwakilishi wao Bwana
Massimiliano Bramucci kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar za kuipatia huduma za Afya Jamii katika masafa yasiozidi
kilomita tano.
“
Nimefarajika na hatua zenu mlizozichukuwa za kusaidia maendeleo ya
Wananchi wetu hasa katika Miradi ya Afya na Elimu jambpo ambalo
umeipunguzia mzigo mkubwa Wizara yetu ya Afya ya kuendelea kusimamia
masuala ya afya hapa Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.
Akizungumzia huduma za Afya Balozi Seif aliwaasa wananchi kuendelea
kuvitumia vituo vya afya kwa kuangalia afya zao na kuachana na kutumia
dawa za miti shamba zisizo na kiwango ambazo kwa kiasi kikubwa huleta
madhara kwa watumiaji hao.
“
Umefika wakati sasa ndugu wananchi wenzangu kuachana na dawa za
kienyeji za miti shamba ambazo hazina kiwango ma rana nyingi huleta
athari katika miili yetu “. Alisisitiza Balozi Seif.
Mapema
Mwakilishi wa Hoteli ya Waride Resort Bwana Massimiliano Bramucci
ambaye ndie mfadhi ya Kituo hicho cha huduma za Waja wazito Pwani
Mchangani amewashukuru wananchi wa Pwani Mchangani kwa ushirikiano wao
uliosaidia kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati.
Bwana Massimiliano katika kushajiisha wananchi hao kuvitumia Vituo
hivyo kwa kupata huduma za afya ameahidi kufanya sherehe kubwa kwa motto
wa mwanzo atakayezaliwa katika Kituo hicho cha huduma za wajawazito cha
Pwani Mchangani.
Akitoa
salamu za Wizara ya Afya Zanzibar Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya
Dr. Jamala Adam alisema ujenzi wa vituo hivyo viwili ni mfano mzuri wa
mashirikiano kati ya wananchi wa Pwani Mchangani na Wawekezaji.
Dr.
Jamala alisema ijenzi wa Vituo hivyo unakwenda sambamba na ile azma ya
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ya
kutangaza huduma za Afya kutolewa bure kwa wananchi wote mnamo mwaka
1965.
Katika
Risala yao Wananchi hao wa Kijiji cha Pwani Mchangani iliyosomwa kwa
niaba yao na Mwalimu Mwinyi Sauti Haji aliiomba Serikali kuangalia
uwezekano wa kuwapatia mafunzo ya Afya Vijana wa Kijiji hicho ili waje
kusaidia kutoa huduma hapo baadaye katika Vituo hivyo.
Mwalimu
Mwinyi Sauti Haji aliushukuru Uongozi wa Hoteli ya Waride Resort na ule
wa Ocean Paradise kwa misaada yao mikubwa ya maendeleo ambayo inakwenda
sambamba na malengo ya Milenia.
Kituo
cha Huduma za Wajawazito cha Kijiji cha Pwani Mchangani pamoja na Kituo
cha Afya viliopo Pacha vimefanikiwa kuwa na Vifaa vya kisasa vya
uchunguzi wa maradhi mbali mbali ikiwemo mashine ya Utra Sound, Chumbna
cha Operesheni mdogo, Maabara pamoja na chumba cha kupumzikia wagonjwa.
Zaidi
ya shilingi za Kitanzania Milioni mia Tisa zimetumika katika ujenzi wa
Vituo vyote viwili ikiwa ni mchango uliogharamiwa na wafadhili wa Hoteli
hizo mbili zilizomo ndani ya Kijiji cha Pwani Mchangani.
Post a Comment