Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipeana mikono na
Msaidizi wa masuala ya Biashara kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi
yenye Makao Makuu yake katika Mji wa Dalien Nchini China { CDIG } ambayo
tayari imeshafungua Tawi lake Dar es salaam Tanzania Bwana Lin Heng. Kati kati yao ni Mwakilishi wa Kampuni ya Billion Resources kutoka nchini Nigeria Bwana Segun Olonade.
|
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za
uwekezaji vitega uchumi kutoka Kampuni mbali mbali za Kimataifa
zinazojihusisha na masuala ya Ujenzi wa miradi tofauti ambao tayari
wameshafungua Umoja wa tawi lao Nchini Tanzania.
Kulia
ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa Kampuni ya Billion Resources Mzaliwa
kutoka Nchini Nigeria Bwana Segun Olonade na Msaidizi wa masuala ya
Biashara kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CDIG Bwana Lin Heng.
Kushoto
yake ni Bwana Kennedy Shine wa Kampuni ya Kemisy Group, Bwana Ron
Adjafary Mthenga wa Kampuni ya Billion Resources na Emmanuel Kawedi wa
Kampuni ya Kemisy Gropu.Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Kampuni
ya Kemisy Group Bwana Kennedy Shine ndani yao kwenye Jengo la Msekwa
Mjini Dodoma. Picha na Hassan Issa wa OMPR, ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Taasisi na washirika wa Maendeleo bado wana fursa nzuri na pana ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo na Kiuchumi.
*********
Alisema fursa hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuleta ustawi bora wa Wananchi sambamba na kuimarisha nguvu za uendeshaji wa Taasisi na Mashirika hayo katika mipango yao ya uzalishaji. Balozi Seif alisema hayo Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa Bungeni Mjini Dodoma wakati akizungumza na Wawakilishi wa Taasisi za uwekezaji vitega uchumi kutoka Kampuni mbali mbali za Kimataifa zinazojihusisha na masuala ya Ujenzi wa miradi tofauti ambao tayari wameshafungua Umoja wa tawi lao Nchini Tanzania.
Alisema Serikali inaendelea na sera na mipango ya ujenzi wa nyumba kwa kushirikiana na washirika wa Maendeleo ili baadaye zikopeshwe au kuuzwa kwa wananachi hasa wale wa kipato cha chini kwa lengo la kuondosha tatizo la makazi ya Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza Kampuni za Kimataifa za Ujenzi za Jamuhuri ya Watu wa China ambazo zinatoa huduma zake katika miradi mbali mbali hapa Zanzibar.
“ Tumejenga imani kubwa kwa Makampuni mengi ya China ambayo yamekuwa yakifanya kazi mbali mbali za Miradi ya Ujenzi kwa umahiri na umakini wakizingatia zaidi muda katika Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba “. Alisema Balozi Seif.
Aliwaomba wawakilishi wa Taasisi na Mashirika hayo ya miradi ya ujenzi kutenga muda maalum wa kutembelea na kukagua fursa zilizopo Zanzibar ili waweze kuwekeza miradi yao ya maendeleo. Balozi Seif alisema Sekta ya Utalii bado ina nafasi nzuri kwa wawekezaji wa Kimataifa kuwekeza miradi yao itakayiosaidia kutoa ajira pamoja na kuongeza mapato ya Taifa.
Akizungumzia suala la huduma za Umeme wa hakiba inapotokezea hitilafu ya uliopo hivi sasa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali Kuu inaendelea kuangalia mazingira ya kuwa na hadhari na suala hilo.
Alisema hivi sasa Kisiwa cha Unguja kinategemea huduma za Umeme za kianzio kimoja tuu cha huduma hiyo kutoka Mjini Dar es salaam wakati Kisiwa cha Pemba kikitegemea huduma hiyo kutokea Mkoani Tanga.
Mapema Msaidizi wa masuala ya Biashara kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi yenye Makao Makuu yake katika Mji wa Dalien Nchini China { CDIG } ambayo tayari imeshafungua Tawi lake Dar es salaam Tanzania Bwana Lin Heng alisema Taasisi yake iko huru kushirikiana na Mashirika ya Kizalendo katika kuendeleza miradi mbali mbali ya Ujenzi.
Bwana Lin Heng alisema Taasisi hiyo inajihusisha zaidi na miradi ya ujenzi wa Bandari, Uwanja wa Ndege, Umeme pamoja na ujenzi wa nyumba ambapo baadhi ya miradi inatekelezwa katika baadhi ya Mataifa Barani Afrika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Wawakilishi wa Taasisi za uwekezaji kutoka Kampuni mbali mbali za Kimataifa zinazojihusisha na masuala ya Ujenzi wa miradi tofauti ambao tayari wameshafungua Umoja wa tawi lao Nchini Tanzania.
|
on Tuesday, March 25, 2014
Post a Comment