Mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayub akifungua mkutano huo
WANAWAKE
11 nchini hupoteza maisha kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa
kizazi kila siku huku wanawake 6000 hugundulika kuwa na ugonjwa wa
saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka .
Mkurugenzi mtendaji
wa T-MARC Tanzania Bi Diana Kisaka aliyasema hayo leo katika ukumbi
wa VETA wakati wa ufunguzi mkutano wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia
na kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi mkoani
Iringa.
Iringa.
Alisema kuwa
jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa takribani wanawake 4000
nchini hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huo ambapo ni
sawa na wastani wa wanawake hao 11 kwa siku hupoteza maisha yao.
Hata
hivyo alisema kuwa takwimu kutoka Hospital ya Ocean
Road zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya vifo hivyo vinavyotokana na
matatizo ya saratani ni wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi , huku
takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa
wote wanmaokwenda kwenye matibabu ya saratani ya malango wa kizazi
fufika Hospital kupata huduma hiyo kwa kuchelewa zaidi.
Alisema
kuwa kwa ujumla ugonjwa wa Saratani ni tatizo kubwa sana
ulimwenguni na hasa katika nchi zinazoendelea ambapo takwimu za
kimataifa zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya watu milioni 5
hugundulika kuwa na saratani na kufanya tatizo hilo kufikia asilimia
29 huku kati yao hupatikana na saratani ya mlango wa kizazi na kwa
bahati mbaya Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la
ugonjwa huo.
Bi Kisaka
alitaja baadhi ya sababu zinazochangia tatizo hili nchini ni
pamoja na ukosefu wa taarifa kuhusu umuhimu wa watu kuchunguza afya
zao mara kwa mara watu wengi husubiri hadi hali yao ya afya
iwe mbaya sana kabla ya kutafuta huduma za uchunguzi na matibabu Hospitalini .
iwe mbaya sana kabla ya kutafuta huduma za uchunguzi na matibabu Hospitalini .
Sababu
nyingine ni pamoja na imani potofu na kukosa taarifa halisi
kuhusu saratani na matibabu ya saratani ,hasa matibabu ya mionzi
,upungufu wa huduma za uchunguzi na matibabu ya saratani ,upungufu
wa wataalam
wa afya pamoja na ufinyu wa bajeti na upungufu wa fedha za kukidhi mahitaji ya huduma za kuzuia na kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi.
wa afya pamoja na ufinyu wa bajeti na upungufu wa fedha za kukidhi mahitaji ya huduma za kuzuia na kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi.
Alisema
kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo T-MARC kama asasi isiyo kuwa
ya kiserikali ambayo inajishughulisha na uboreshaji wa afya
ya watanzania kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara ya Afya
na
ustawi wa jamii pamoja na wadau mbali mbali wa sekta ya umma
,sekta binafsi ,wadau wa kimataifa ,asas za kijamii na watanzania wote
kwa ujumla kwa kuanza kupambana na tatizo hilo.
Na Francis Godwin Blog
Post a Comment