Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
yatumia zaidi ya bilioni 500 katika utekeleaji wa miradi ya Matokeo
makubwa sasa katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2013.
Hayo
yamesemwa na Kiongozi wa Miradi ya Matokeo makubwa sasa (BRN) wa Wizara
ya fedha Bw. Emmanuel Tutuba wakati wa mkutano na waandishi wa A
Akieleza
zaidi bw. Emmanuel amesema Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi
mbalimbali chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ambapo alitaja
miradi hiyo kuwa ni Elimu iliyopewa jumla ya shilingi bilioni 8.3 na
miradi ya maji imepewa shilingi bilioni 86.
Alitaja
miradi mingine kuwa ni ya kilimo ambayo imepewa jumla ya shilingi
bilioni 10.2 na miradi ya uchukuzi iliyopewa shilingi bilioni 146.6.
Aidha
Bw. Emmanuel alitaja miradi mingine kuwa ni ya nishati iliyopewa jumla
ya shilingi bilioni 339.4 ili kusaidia katika kuimarisha Sekta ya
nishati ili kusaidia ukuaji wa uchumi nchini.
Wakati
huo huo Bw. Emmanuel alisema katika kipindi cha julai hadi Disemaba,
2013 jumla ya shilingi bilioni 215 zimekusanywa kutokana na vyanzo vipya
vya kodi vilivyoibuliwa na maabara ya matokeo makubwa sasa.
Jumla
ya shilingi bilioni 10.9 zimekusanywa kutokana na utekelezaji wa hatua
za kuongeza mapato yasiyo ya kodi kwa kutoa leseni za kuvuna mazao ya
misitu na vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada.
Uboreshaji
wa kukusanya kodi ya majengo na kodi ya ardhi katika Halmashauri za
manispaa za Temeke, Ilala, na Kinondoni unaendelea vizuri ikiwa ni moja
ya chanzo kipya cha mapato ambapo halmashauri hizo zimetumika kama
sehemu za majaribio kabla ya kuenezwa katika halmashauri zote nchini ili
kuongeza mapato.
Hata
hivyo Serikali imeamua kuanzisha utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi yenye thamani ya shilingi trilioni 6 hadi
kufikia mwaka 2015/16.
Miradi
ya awali ambayo imebainishwa kuanza kutekelezwa kwa ubia ni ujenzi wa
barabara ya Dar es salaam hadi Chalinze, uendeshaji wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka jijini Dar es salaam na ujenzi wa kituo cha kufua umeme
cha Kinyerezi.
Naye
Mwenyekiti wa mradi wa matokeo makubwa sasa toka Wizara hiyo Bi Alvera
Ndabagoye alitoa wito kwa vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi
kuhusu miradi ya matokeo makubwa sasa ili kuongeza ushiriki wa wananchi
katika kukuza uchumi.
Tekeleza
kwa matokeo makubwa sasa (BRN) ni utaratibu unaotumiwa na Serikali
katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa vipaumbele katika Sekta
sita zinazolenga kuongeza ukuaji wa uchumi ambazo ni Elimu, Maji,
Nishati, Kilimo, Uchukuzi na Afya kwa kushirikisha wadau wote.
Post a Comment