Baadhi ya washiriki wa warsha.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akihutubia katika warsha.
Wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya DAWASA, watumishi wa Wizara ya Maji, DAWASA, DAWASCO na Bonde la Wami Ruvu.
Mwenyekiti wa mkutano, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko na Makamu Mwenyekiti ya Bodi ya DAWASA, Said El Maamry wakisikiliza mjadala katika warsha hiyo.
……………………………………………………………………..
Warsha
ya wadau ya kujadili taarifa ya tathmini ya athari za kijamii na
mazingira ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda imefanyika jana katika
Hoteli ya Nashera, mjini Morogoro.
Warsha
hiyo imeshirikisha wadau wote wa sekta ya maji ngazi ya Serikali Kuu
mpaka Serikali za Mitaa; ilijumuisha Wizara ya Maji, Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Kampuni ya Maji Safi na
Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), Baraza la Taifa la Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) na viongozi wa mkoa wa Morogoro.
“Wazo
la kujenga Bwawa la Kidunda kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwa
pamoja na kuboresha huduma ya maji ya jiji la Dar es Salaam na miji ya
Kibaha na Bagamoyo ni la muda mrefu. Hivyo, warsha hii ni mwendelezo wa
hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ili kuwezesha mradi wa
ujenzi wa Bwawa la Kidunda”, alisema mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Joel Bendera.
Mkuu
wa Mkoa aliongeza yapo manufaa mengi na makubwa yanayotokana na matumizi
sahihi ya Bwawa la Kidunda, barabara na umeme baada ya ujenzi wa mradi
huu kukamilika na kuleta maendeleo makubwa nchini.
“Bwawa
la Kidunda ni mhimili wa vyanzo vya Ruvu Juu na Ruvu Chini, na ili
uzalishaji wa maji kupitia mitambo ya Ruvu Chini uwe mzuri zaidi hatuna
budi kujenga Bwawa la Kidunda. Aidha, kabla ya utekelezaji wake, ni
muhimu kujadili athari zake kijamii na kimazingira na kupata ufumbuzi
utakaopendekezwa na wataalamu”, alisema Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA,
Hawa Sinare.
Pia,
Mwenyekiti wa warsha hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Bashir
Mrindoko alisema anawahakikishia wananchi kuwa athari zote na changamoto
nyingine zitakazoainishwa na Mtaalamu Mshauri zitachukuliwa hatua
sahii. Juhudi na tahadhari zimechukuliwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi
atakayeathirika anatendewa haki kwa mujibu wa sheria.
Lengo
la warsha hiyo ni kutathmini athari za ujenzi wa barabara ya Ngerengere
mpaka Kidunda, mtambo mdogo wa kuzalisha umeme kutoka Kidunda hadi
Chalinze kijamii na kimazingira. Warsha hiyo ya siku moja iliandaliwa na
(DAWASA) kushirikiana na Wizara ya Maji.
Post a Comment