Katibu
Mkuu CCM,Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga
wakiingia kwenye Uwanja wa Mkutano Kata ya Nzihi Jimbo la Kalenga,Pia
walichukua muda kusalimiana na Wananchi wa Kata ya Nzihi waliokuwa na
Shauku ya Kusikia maneno ya Viongozi hawa wa Chama Cha Mapinduzi.Mapokezi Mazito ya Mgombea wa CCM Ndugu Godfrey William Mgimwa wakati wa Kufunga Kampeni hapa Kalenga hii leo.Katibu Mkuu CCM akifurahia Jambo na
Naibu katibu Mkuu-CCM Bara Mh.Mwigulu Nchemba na Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa.Msanii
Dokii ambaye ni kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akiimba wimbo
maalumu unaomuhusu Mgombea wa CCM Jimbo La Kalenga Ndugu Godfrey William
Mgimwa na anavyotakiwa Kutatua changamoto za Wanakalenga na Kutekeleza
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kama alivyokuwa Mbunge wa CCM aliyefariki.Chifu
Mkwawa akizungumza na Wananchi wa kata ya Nzihi,Kubwa amewaomba
Kumpigia Kura Godfrey William Mgimwa Kwa sababu yeye Kama Chifu amekuwa
bega kwa bega na Chama Cha Mapinduzi na ameshuhudia Maendeleo Makubwa
yakifanywa na CCM hususani Ujenzi wa Hostel za Wasichana
Mashuleni,Umeme,Vituo vya AFya na Barabara zinazopitika wakati wote.Mh.Kangi
Lugola akiwaomba Wanakalenga Kumchagua Godfrey WIlliam Mgimwa hapo
Kesho kwasababu ni Kijana na ananidhamu,Amesema hahitaji kuona Wananchi
wanapoteza Muda kuchagua watu wanamtusi Rais wa Nchi,Wanatoka Bungeni
wakati wa Bajeti na Wamegeuza chama cha Ukoo.Katibu wa UVCCM Taifa Ndugu Sixstus Mapunda akiwahakikishia Wanakalenga Usalama wao katiaka Zoezi Zima la Kupiga Kura.Katibu
wa CCM Mkoa Wa Mtwara Ndugu.Akwilombe akitoa wito kwa Wanakalenga
kuacha kusikiliza Propaganda eti Godfrey William Mgimwa anarithi
Ubunge.Amewambia Godfrey amepatiakana katika Mchakato halali wa Kura za
Maoni tena ukihusisha wagombea 9.Wale wanaosema Kuwa Mgimwa anarithi
Ubunge ni Waongo kwa sababu wao Wenyewe Chama Kizima ni Mtu na Mdogo Mtu
au Mkwe na Mkwe au Baba na Mtoto(ameorodhesha U-familia ndani ya
Chadema).
Naibu
katibu Mkuu CCM-Bara Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa
Kata ya Nzihi hii leo wakati wa Kufunga Kampeni za Ubunge Jimbo la
Kalenga.
Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh.Mwigulu Nchemba amewasihi Wanakalenga(kata ya
Nzihi)Kuendeleza Wembe wa Kuikataa CHADEMA kabisa kabisa katika Nchi hii
kwasababu wamekuwa Vinara wa Kusababisha Mauaji na Machafuko ya Amani
katika Miji yetu.Pia amesisitiza kuwa Uchaguzi huu Mdogo haubadirishi
Serikali,Kwasababu wenye Ilani ni CCM na Ilani Inayotekelezwa Kalenga
niya CCM,Ametolea Mfano kuwa Itawekazana Vipi Amefariki Muumini wa
Kiislamu eti Unamwita Askofu akaendeshe Mazishi,au Amefariki Mkristo
unamuita Shekhe akaendeshe Misa ya Mazishi??.Ni jambo lisilowezekana
hata kidogo,CCM ndio wenye Ilani Inayotekelezwa hivyo Mbunge anayetakiwa
kusimamia Ilani hiyo ni Godfrey William Mgimwa wa Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu CCM Taifa Kanali Mstaafu Kinana akifunga rasmi Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi,amewaomba sana Wanakalenga keuendelea Kuwa na Imani na Chama Cha Mapinduzi na Kesho Wananchi wajitokeze wakapige Kura kumchagua Godfrey William Mgimwa iliaendelee kutekeleza pale alipaochia Mbunge aliyefariki.
Katibu Mkuu CCM Taifa Kanali Mstaafu Kinana akifunga rasmi Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi,amewaomba sana Wanakalenga keuendelea Kuwa na Imani na Chama Cha Mapinduzi na Kesho Wananchi wajitokeze wakapige Kura kumchagua Godfrey William Mgimwa iliaendelee kutekeleza pale alipaochia Mbunge aliyefariki.
Picha na Maelezo na Sanga Festo wa Habari Kwanza Media/Blog
Post a Comment