Na Magreth Kinabo- Maelezo
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge Maalum la Katiba Machi 19,mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa bunge hilo Samwel Sitta mjini
Dodoma baada ya kusitisha shughuli za kuapisha wajumbe wa bunge hilo.
Mwenyekiti
huyo alisema Rais Kikwete atalihutubi bunge hilo mara baada ya
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiiko ya Katiba Jaji Joseph Warioba
kuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba mpya Machi 17,mwaka huu majira
ya saa10.00 jioni.
Aidha
Sitta aliongeza kuwa wajume wabunge hilo ambao hawajaapishwa
wataendelea kuapishwa Machi 17,mwaka huu mara baada ya kuanza kwa kikao
cha bunge hilo kuanza saa 3:00 asubuhi.
Alifafanua kuwa wajumbe wa bunge hilo wanatarajiwa kupewa semina ya juu ya mabadiliko ya katiba mpya kutoka ujumbe maalum nchini Kenya Machi 8,mwaka huu.
Alifafanua kuwa wajumbe wa bunge hilo wanatarajiwa kupewa semina ya juu ya mabadiliko ya katiba mpya kutoka ujumbe maalum nchini Kenya Machi 8,mwaka huu.
Post a Comment