Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 8 mwaka huu) kwa mechi
tatu ambapo Coastal Union itaumana na Ashanti United kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Ruvu
Shooting itaikaribisha Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi
mkoani Pwania wakati Mbeya City itacheza na Rhino Rangers kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za Jumapili (Machi 9 mwaka huu) ni Tanzania Prisons na Simba kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, na JKT Ruvu na Mtibwa
Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Post a Comment