Na Jovina Bujulu ,MAELEZO DODOMA
Serikali
itaendelea kuchukuwa hatua za utekelezaji katika maeneo ya kijamii ili
kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Dkt. Pindi Chana hivi karibuni Mjini Dodoma.
Akizataja
hatua hizo hizo Dkt. Pindi alisema kuwa serikali imemekuwa
ikiwajengea wanawake uwezo wa kisheria ili kuweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika maisha na jamii kwa ujumla.
“Sheria
kadhaa zimekuwa zikitungwa na nyingine zikifanyiwa marekebisho, ikiwemo
sheria ya makosa ya kujamiiana ya Mwaka 1998, sheria ya Ajira na
Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009
na hii yote ni kuhakikisha tunawajengea wanawake mazingira bora” Alisema
Dkt. Pindi.
Aidha,
Dkt. Pindi aliongeza kuwa kumekuwepo na ongezeko la ushiriki wa
wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi, Ongezeko hilo linatokana na
marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1995
ambapo viti maalum viliongezwa na kuwa asilimia 15 kwa Tanzania bara na
asilimia 20 kwa upande wa Zanzibar.
Pia
Dkt. Pindi alisema kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo ya
wanawake unaotoa mikopo ya uanzishwaji wa biashara na shughuli nyingine
za kiuchumi ili kuwawezesha wanawake nchini.
Aliongeza
kuwa serikali imeandaa sera ya mitaji midogo midogo ya mwaka 2000
ambayo imeweka mazingira mazuri kwa taasisi binafsi za fedha kama
PRIDE, FINCA, BENKI YA WANAWAKE NA CATSBY kutoa mikopo kwa wanawake.
Madhumuni
ya kuazimisha siku ya Wanawake duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu
umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa unaofanywa na
wanawake katika kuleta maendeleo na jitihada zinazofanywa na Serikali
katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii.
Post a Comment