Mheshimiwa
Dk. Pindi Chana (Mb), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto afungua Mkutano Mkuu wa siku mbili wa Baraza la Watoto la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania mkoani Morogoro Tarehe 11 hadi 12 Machi, 2014.
Mkutano huo wa siku mbili unajumuisha wajumbe wa Mabaraza ya watoto
kutoka Mikoa mbalimbali nchini.
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali katika kusimamia utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu
maendeleo na upatikanaji wa haki za watoto kote nchini. Mojawapo ya
jitihada hizi ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wanapata fursa ya
kushiriki na kushirikishwa katika masuala mbalimbali yanayowahusu. Hivyo
basi, uanzishwaji wa Mabaraza ya watoto ni mojawapo ya jitihada za
Wizara na wadau mbalimbali wa watoto kuhakikisha kuwa watoto wanapata
fursa ya kukutana na kujadili mambo mbalimbali ya utekelezaji wa
mikataba ya kitaifa na kimataifa inayohusu haki na ustawi wao
inavyotekelezwa hapa nchini.
Katika
miaka ya hivi karibuni, matukio mengi ya unyanyasaji, udhalilishaji na
ya ukatili dhidi ya watoto yanajitokeza katika jamii hapa
nchini. Mengine yanasikika na kusomwa katika Vyombo vya Habari, licha
ya yale ambayo hayatolewi taarifa. Kwa ujumla matukio haya yote
yanaonesha jinsi haki za msingi za watoto zinavyokiukwa.
Hivyo
basi, katika kukabiliana na hali hii Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali zinazolenga kuhakikisha
kuwa jamii inaelimishwa vya kutosha ili itambue na kuthamini utu na
haki za watoto. Mojawapo ya jitihada hizo ni:-
Kuandaa Mpango Kazi wa miaka mitatu (2013 – 2016) wa kuzuia na kushughulikia masuala ya ukatili dhidi ya watoto hapa nchini.
Kuanzisha
Mtandao wa Mawasiliano wa Kusaidia Watoto nchini Tanzania (Tanzania
Child Helpline). Mtandao huu utatoa fursa kwa watoto na au watu wazima
kwa niaba ya watoto kuripoti vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili
kuwezesha waathirika wa ukatili kupata msaada/huduma kwa wakati muafaka
na pia kuhakikisha kuwa wahusika wa uhalifu huo wanafikishwa katika
mamlaka husika.
Kuwawezesha
watoto kupitia wawakilishi wao kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa
Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kuratibu
uandaaji wjenda ya Watoto ambao imejikita katika maeneo kumi ya
uwekezaji kwa watoto hapa nchini ambayo ni kuwekeza katika kuokoa maisha
ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza kwenye
usafi na udhibiti wa miundombinu ya maji taka katika shule na kwenye
huduma za afya, kuwekeza katika kumuendeleza mtoto akiwa bado mdogo,
kuwekeza katika elimu bora kwa wote, kuwekeza katika kuzifanya shule
kuwa mahala pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda watoto wachanga na
wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza mimba za utotoni,
kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu , udhalilishaji na unyonyaji
na mwisho kuwekeza kwa watoto wennye ulemavu.
Post a Comment