BABU
mwenye umri wa miaka (80), Benedict mkazi wa Tandika Kilimahewa, jijini
Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumbaka mjukuu wake wa kike (jina
linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka (6). Tukio hilo la kuhuzunisha
linadaiwa kutokea Machi 8, mwaka huu usiku wakati babu na mjukuu wake
huyo wakiwa wamelala pamoja chumbani kwake.
Akizungumza
na mwandishi wetu, jirani wa babu huyo ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini alidai kwamba aliyegundua mtoto huyo kabakwa ni
mjumbe wa nyumba kumi wa eneo analoishi mtuhumiwa anayefahamika kwa jina
la Bibi China.
“Sisi
hatukuwa na habari ila mjumbe wetu aliposikia watoto wakisema nguo ya
ndani ya mwenzao (mtoto aliyebakwa) ilikuwa na damu alimwita na
kumkagua, alipomuuliza alipatwa na nini akamwambia babu yake alimfanyia
mchezo mbaya,” alidai jirani huyo.
Aliongeza
kuwa, baada ya kumhoji kwa kina, mtoto huyo alisema kuwa usiku akiwa
amelala na babu yake alimvua nguo na kuanza kumfanyia kitendo hicho.
Jirani
huyo alidai kwamba, mtoto aliwaambia kutokana na maumivu makali
aliyopata alipiga mayowe ya kuomba msaada lakini babu yake aliongeza
sauti ya redio hadi mwisho ili watu wasisikie.
Mjumbe wa
nyumba kumi wa mtaa huo, Bibi China alikiri kutokea tukio hilo na
kuongeza kuwa mtuhumiwa ambaye hana mke alikuwa akilala kitanda kimoja
na mjukuu wake huyo.
Mtoto aliyefanyiwa unyama huo akizungumza kwa huzuni na paparazi wetu alisema:
“Nilikuwa
nimelala nikashtuka navuliwa nguo na babu na kuanza kunibaka, ilikuwa
usiku wa manane, nililia lakini yeye aliongeza sauti ya redio ili watu
wasisikie nikanyamaza, asubuhi bibi ndiyo akaniona halafu mama
akanipeleka hospitali.”
Mama mzazi wa mtoto huyo, Sikwambii Mateo akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Kitendo
alichofanyiwa mwanangu na baba yangu mzazi kimeniumiza sana na imekuwa
vigumu kuamini kwa umri aliokuwa nao kama angeweza kufanya kitendo cha
kikatili kwa mjukuu wake na kudai anasingiziwa, nilipompeleka Hospitali
ya Temeke alipochunguzwa alikutwa na manii,” alisema mama huyo.
Babu huyo mpaka sasa anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Kilimahewa kwa RB namba KLH/RB/236/2014 KUBAKA.
>>GPL
Post a Comment