Raisi wa klabu bingwa ya Bayern Munich Uli Hoeness amejiuzulu kwenye
nafasi yake ya uraisi wa klabu hiyo na amesema ameamua kutokata rufaa
dhidi ya hukumu aliyopewa.
Hoeness, mmoja watu wazito katika soka nchini Ujerumani, alihukumiwa
kwenda jela miaka mitatu na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa
kodi .
Hoeness alisema kupitia taarifa fupi iliyochapishwa kwenye mtandao wa
klabu ya Bayern kwamba amefikia maamuzi hayo baada ya kuzungumza na
familia yake na akawaelekeza wanasheria wake wasikate rufaa.
Post a Comment