Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Jaji Mst.Damian Lubuva ametoa wito kwa
wananchi walio jiandikisha Kupiga Kura Katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Kalenga utakao fanyika tarehe 16 machi 2014, Kujitokeza kwa wingi
kwenda kwenye Vituo vilivyopangwa kwa ajili ya Kupiga Kura ili
kutekeleza haki yao ya katiba ya kumchagua mtu anayemtaka kuwa kiongozi
wao.
Jaji Mst.Lubuva amesema, vituo vya kupiga kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi jioni.
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imewakumbusha wananchi wa Kimbo la Kalenga kubeba Kadi
ya Mpiga kura kwa kuwa bila ya kadi ya Mpiga kura hatoruhusiwa kupiga
kura.
Ameongeza
kuwa, wagonjwa wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake
wajawazito, wanaonyonyesha na wazee hawatatakiwa kujipanga kwenye mstari
bali wataelekezwe kwenda moja kwa moja kupiga kura.
Amesema,
mpiga kula anayeishi na ulemavu wa kutoona ataruhusiwa kuja kituoni na
mtu aliyemchagua mwenyewe, na mtu mmoja anaweza kumsaidia mpiga kura
mmoja tu, labda kama wapo wapiga kura zaidi ya mmoja kutoka katika
familia moja.
Aidha,
Tume imesisitiza mambo muhimu vikiwemo vyama vya siasa kuweka mawakala
wake katika vituo vyote 216 vya kupiga kura na kujumlisha kura pamoja na
mawakala kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Ameongeza
kuwa mpiga kura anatakiwa kupiga kura katika kituo alichoandikishwa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuzingatia maadiri mara baada ya mpiga kura
kupiga kura anatakiwa kurejea nyumbani kwa kuwa vyama vya Siasa
vitakuwa vimeweka mawakala wake ambao watalinda maslahi ya vyama husika
na wagombea wao.
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inamtaka mtu kupiga kura kwa Siri na asishawishiwe na
mtu yoyote kueleza nani amempigia kura na ni kosa la Jinai kumkataza mtu
kwenda kupiga kura kwani ni haki yake ya kumchagua mtu anayemtaka kuwa
kiongozi wake.
Matokeo hayo ya Uchaguzi utakaofanyika kesho 16 machi 2014 yatatangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo.
Hata hivyo tume inamatumaini yakuwa hali ya amani na utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa, itaendelea kudumishwa.
Post a Comment