Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RIDHIWANI KIKWETE HAKUNA KULALA .... AENDELEA NA KAMPENI KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

 



Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014, wakati akiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.



Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa wakazi wa Kijiji cha Miono,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano ya Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.

Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi (kulia) akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kabla ya kumpatia kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wanakijiji wa Kimange


 Picha zote na Othman Michuzi.



Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete pamoja na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi wakiwa na Mama wa Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Chalinze (aliefariki Dunia),Marehemu Said Bwanamdogo wakati walipofika kumjulia hali nyumbani kwake Kijijini Miono,Bagamoyo leo Machi 15,2014.

Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Kumpigia debe Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo,Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani),uliofanyika leo Machi 15,2014 kwenye Kijiji cha Kimange.

"Kinamama huko,inamaana hakuna vigelegeleeeee .....???" hivyo ndivyo alivyokuwa akiuliza Diwani wa Kata ya Kimange,Hussein Hading'oka (pichani) wakati alipokuwa akimwaga sifa kede kede kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top