Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.
Athari
za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata
Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.
Wanawake
wengi wanaofanya kazi huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi
wanapofika umri a miaka 35 badala ya kuzaa wakiwa na umri wa miaka
24-28.
Mtaalamu
wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu
hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma
masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha
kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''
Bwana
Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au
uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi
au HIV.
Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.
Post a Comment