Matukio
ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China huku wakihusishwa na biashara
ya dawa za kulevya yamekua yakitangazwa mara kwa mara huku wengi wao
tukipata taarifa za kuwa hukumu yao wamekuwa wakihukumiwa kunyongwa.
Katibu
Mkuu wa mambo ya Nje John Haule ametaja jumla ya watuhumiwa
waliokamatwa kwa kesi ya madawa ya kulevya>>’Tuna Watanzania wengi
tu ambao wapo kwenye magereza kule nchini China tumeshindwa kwa haraka
haraka kupata idadi ya waliojihusha na shughuli ya dawa za kulevya’
‘Katika
Magereza ya China mpaka February tumepewa taarifa na Mamlaka za China
kwamba wapo Magerezani Watanzania 177 na katika ya hao 15 wamehukumiwa
kunyongwa kutokana na biashara hiyo ya dawa na kukamatwa na dawa hizo
lakini niseme tu wenzetu wa Serikali ya China wanatuthamini sana kama
sisi tunavyowathamini’
‘Lakini wenzetu wanathamini zaidi mahusiano yetu na ndiyo maana hata
wale wachache Watanzania waliohukumiwa kunyongwa kutokana na makosa hayo
waliyotenda kule hawajanyongwa mpaka leo na hatutegemei kama
watanyongwa sana sana watafungwa kifungo cha maisha’.
Post a Comment