Ukuaji
wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Msichana akili
yake huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo
tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba pindi
wanapolea mtoto wa kike husogea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea
mtoto wa kiume,” anasema Tuzie.
Imekuwa
ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika Afrika kuwa
msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa ni
vigumu kuelewana na kuheshimiana.
Dhana
hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na
mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na akili iliyokomaa zaidi
kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya umeipa uzito nadharia
yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana hukomaa haraka kuliko wa
mvulana.
Watafiti
kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea
sababu za wasichana wadogo kuonekana kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao
wa kiume wenye umri sawa.
Wanasayansi
walitumia kipimo maalumu kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu 121
waliokuwa na umri kuanzia miaka minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu
yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe huanza kati ya miaka 10 kwa
msichana, huku mvulana huchukua muda mrefu kuanzia miaka 11 mpaka 20.
Dk. Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti, anasema: “Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.
“Kwa
kawaida hata katika utambuzi, imeonekana kwamba msichana ana uwezo wa
kushika mambo mengi zaidi kuliko mvulana, ndiyo maana katika nchi za
Afrika mtoto wa kike anapika, anajaribu kutekeleza majukumu ya nyumbani
kama mama yake, bado shuleni atafanya vizuri, lakini si kwa mvulana.
Akishazongwa na mambo mengi hupunguza morali shuleni.”
Dk.
Kaiser anafafanua kuwa hatua za ukuaji wa mtoto wa kike ni za haraka
ukilinganisha na wa kiume. Hii inatokana na mfumo wa kike. Binti hukua
haraka kutokana na homoni zake mwilini na pia akishabalehe ndipo anakuwa
na uelewa mpana kutokana na via vyake vya mwili kumruhusu kubeba
ujauzito.”
Wataalamu nchini
Tuzie
Edwin, ambaye ni msemaji wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Kituo cha
Huduma ya Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH), anasema mtoto wa
kike huanza kupevuka kiakili ndani ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
“Ukuaji
wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Akili ya
Msichana huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo
tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba wakati
wanapomlea mtoto wa kike, huongea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea
mtoto wa kiume,” anasema Tuzie na kuongeza:
“Msichana
hutambaa na kutembea haraka zaidi ukilinganisha na mvulana, hata katika
kuongea. Pia huwa na uelewa mpana wa mazingira, anakuwa mwepesi kuanza
kutumia choo mapema na ana kumbukumbu kwamba hivi sasa anahitaji
kujisaidia na pia huanza kujitegemea ndani ya miaka miwili ikilinganisha
na wa kiume,” anasema Edwin.
Anasema
msichana huwa mwepesi katika kuwasiliana na pia huweza kuanza
kushirikishwa katika baadhi ya mambo, kama kutumwa dukani mapema zaidi
ukilinganisha na mvulana.
“Msichana
pia anawahi kupevuka ukilinganisha na mvulana, lakini akishabalehe tu
ubongo wake hukomaa haraka na hapo ndipo maumbile yake yanapoanza
kujitengeneza mapema kwa ajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito
wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua kwa nafasi kubwa kipindi
hiki, ukilinganisha na mwanamume ambaye ni hadi miaka 10 baadaye,”
anasema Edwin.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sayansi katika Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk.
Elifatio Towo anasema mtoto yeyote ana uwezo wa kukua kwa haraka zaidi,
kutokana na namna mzazi anavyomlisha na haina tofauti na jinsi yake.
“Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.
Kunyonyesha
ndiyo sababu pekee inayowafanya watoto akili zao zikue kwa haraka
zaidi. Lakini ikumbukwe kwamba watoto wa kike huwa na busara zaidi
katika baadhi ya mambo na katika kufanya uamuzi ikilinganishwa na wa
kiume,” anasema na kuongeza:
“Huyu
anaweza kufikiria makubwa zaidi ya umri alionao, lakini mara nyingi
inatokana na maumbile kwamba yeye ni mwanamke hivyo kupevuka na anakuwa
tayari kubeba ujauzito, mwili wake unajitengeneza wenyewe,” anasema Dk.
Towo.
Wasemavyo wazazi
Maimuna
Jitegemee, mama mwenye watoto watatu, anasema “Binti yangu niliweza
kumwachia nyumba akiwa na umri wa miaka 13 tu, niliweza kusafiri na
kurudi. Hata hivyo hali imekuwa tofauti kwa mtoto wangu wa kiume, kwani
licha ya kwamba dada yake yupo chuoni hivi sasa, siwezi kumwachia nyumba
japokuwa ana umri wa miaka 15.”
MWANANCHI
Post a Comment