UPUNGUFU
wa nguvu za kiume ni hali ambayo mwanaume au mvulana anapungukiwa au
kukosa kabisa nguvu za kusimamisha viungo vyake wakati wa tendo la
kujamiiana.
Pia
inaweza kuwa ni hali ya mwanaume kuwahi kumaliza wakati wa tendo, au
kuwa na nguvu hafifu. Utafiti unaonesha kuwa wanaume wengi duniani
wanasumbuliwa na tatizo hili ingawa hakuna uwazi wa kutosha wa
kulielezea tatizo lenyewe.
Idadi
kubwa ya wanaume wana nguvu ndogo, nguvu ambayo haikidhi matakwa ya
wenzi au wake zao, huku idadi nyingine kubwa wakiwa hawana kabisa nguvu
hata kidogo.
Inaelezwa
kuwa tatizo hili limesababisha ndoa nyingi kuvurugika na limesababisha
maumivu makubwa kwa watu ambao wako kwenye uhusiano.
Watafiti wa mambo ya uhusiano na mapenzi wamejaribu kutafuta vyanzo
mbalimbali vya tatizo hili na mbinu za namna ya kulitatua. Licha ya
kiusababisha ndoa nyingi kuvurugika inaelezwa kuwa tatizo hili
limepunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wa wanaume kujiamini na kushusha
ufanisi wao majumbani mwao na sehemu za kazi.
Watafiti mbalimbali wamejaribu kwa miaka mingi kutafuta tiba ya kudumu
ya tatizo hili. Miongoni mwa watafiti ambao wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuwarudishia wanaume uwezo wao, ni Daktari Arnold Kegel.
Daktari huyu aligundua aina ya mazoezi ambayo yamethibitishwa
ulimwenguni kote kuwa na uwezo mkubwa wa kumrudishia mwanaume nguvu
zake, hata yule ambaye hakuwa nazo kabisa (hanithi).
Mazoezi hayo yamepewa jina la mgunduzi wake na yanafahamika duniani kote kwa jina la Kegel.
KEGEL NI NINI?
Kama
nilivyoeleza , haya ni mazoezi maalum ambayo huhusisha misuli ya Pelvic
inayopatikana kwenye eneo lililozunguka viungo vya uzazi vya mwanaume,
kwa upande wa ndani wa mwili.
Post a Comment