Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu (kushoto) akiwasilisha kwa
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, utambulisho wa makampuni
ya Uturuki ambayo yamefungua ofisi hapa nchini kwa lengo la kushiriki
katika kazi za kandarasi za ujenzi hapa nchini.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipitia baadhi ya nyaraka
zilizowasilishwa na makampuni ya kandarasi kutoka Uturuki. Wengine
katika picha (kutoka kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamhanga,
Katibu Mkuu Alhaj Mussa Iyombe na kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu
Bw.
Kursat Durak (aliyenyoosha mkoni) kutoka Kampuni ya CEYTUN ya Uturuki
akifafanua jambo. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu, Bw. Hassan Tunk Makamu Mwenyekiti
wa Kampuni ya CEYTUN na kushoto kabisa ni Bw Remzi Demircan Mbia wa
Kampuni ya KAYA.
Kampuni
kadhaa kutoka nchi ya Uturuki zimeanza kuingia Tanzania ili kushiriki
katika kazi za ujenzi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. Kukua kwa
sekta ya ujenzi kumekua ndiyo kivutio kikuu kilichozifanya kampuni hizo
kuonyesha nia ya kufungua ofisi zao hapa nchini.
Wakizungumza
katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
walipomtembelea ofisini kwake, wawakilishi kutoka Kampuni Kampuni tatu
tofauti wamempongeza Waziri huyo kwa jinsi anavyosimamia sekta hiyo ya
ujenzi kiasi cha kuanza kuvutia makampuni makubwa kutoka nje.
“Tumekuwa
tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa
kadhaa barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania ni nchi inayofanya
vizuri katika upande huo” alibainisha Bw. Orhan Babaoglu ambaye ni
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki.
Mwakilishi
mwingine kutoka Kampuni ya CEYTUN ya huko huko Uturuki Bw. Kursat Durak
amebainisha kuwa, utendaji wa kampuni za Kituruki unafahamika duniani
kote, hivyo ujio wao unalengo la kuamsha ushidani wa ubora lakini pia
kuona kuwa gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinathibitiwa kwa kuwa
na washindani kutoka maeneo tofauti.
Mhe.
Magufuli kwa upande wake wakati akiwakaribisha amewataka kuzingatia
sheria na taratibu zinaoongoza shughuli za kandarasi hapa nchini. Waziri
Magufuli aliwajulisha kuwa, mbali na kazi za kawaida za kandarasi kwa
hivi sasa kuna miradi kadhaa mikubwa inayokusudiwa kuendeshwa kwa
kushirikisha sekta binafsi hivyo hiyo pia ni fursa wanayoweza
kujishughulisha nayo hapa nchini.
Post a Comment