Rais
wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(kulia vazi jeupe) akikagua
Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa Magereza Wahitimu wa taaluma ya
Uaskari Magereza Nchini Msumbiji katika Sherehe za kufunga Mafunzo hayo
zilizofanyika Machi 07, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza kilichopo
Maputo, Msumbiji ambapo Nchi mbalimbali za Afrika zilialikwa zikiwemo
Afrika Kusini, Zambia, Namibia, Zimbabwe, Swaziland pamoja na Tanzania.
Jumla ya Wahitimu Maafisa 430 wamehitimu vyema mafunzo hayo ya Uaskari
wa Magereza. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa nne toka
kulia) akiwa meza Kuu pamoja na Wakuu wa Magereza toka nchi mbalimbali
za Afrika katika Sherehe za kufunga rasmi Mafunzo ya taaluma ya Uaskari
Magereza kwa Maafisa Magereza wa Msumbiji. Mgeni rasmi katika hafla hiyo
alikuwa ni Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(wa tatu toka
kulia) ni Kamishna wa Magereza nchini Zambia, Percy Chato.
Gadi
ya Maafisa Magereza wa Msumbiji Wanaume wakipita kwa mwendo wa haraka
wakitoa heshima mbele ya Mgeni rasmi, Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando
Emilio Guebuza katika hafla fupi ya ufungaji Mafunzo ya taaluma ya
Uaskari Magereza kwa Maafisa 430 wa Magereza yaliyofanyika Machi 07,
2014 Maputo, Msumbiji.Kamishna
Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja akisalimiana kwa
kushikana mikono na Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(kama
wanavyoonekana katika picha) baada ya hafla fupi iliyotanguliwa na
Gwaride Maalum katika Sherehe za kufunga rasmi Mafunzo ya taaluma ya
Uaskari Magereza ambapo jumla ya Maafisa Magereza 430 wamehitimu taaluma
hiyo Machi 07, 2014 Maputo, Msumbiji (kulia pembeni kwa Jenerali Minja)
ni Waziri wa Sheria Nchini Msumbiji, Mhe. Bervinda Levi.Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa nne toka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya
Urekebishaji/Magereza Afrika, Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
Nchini Msumbiji pamoja Maafisa Magereza Wahitimu wa Kozi namba 08 ya
Mwaka 2014 ya taaluma ya Magereza (upande wa kulia). Wa tano toka kulia
ni Kamishna wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tano toka kushoto)
ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael
Hamunyela(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Post a Comment