Uzinduzi
wa taasisi ya marehemu Steven Kanumba ijulikanayo kwa jina la Kanumba
The Great Foundation utafanyika Aprili 7 kwenye ukumbi maarufu wa Dar
Live uliopo Mbagala, jijini.Uzinduzi huo utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili tokea kufariki kwa marehemu Kanumba ambaye alifariki dunia Aprili 7.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora
Mtegoa alisema kuwa wameamua kuanzisha taasisi hiyo ili kuendelea
kumuenzi mtoto wake na kuendeleza kile ambacho alikuwa akikifanya wakati
wa uhai wake.
Alisema
kuwa taasisi yao itajihusisha na utoaji wa elimu, kusaidia watoto
yatima, kuibua vipaji vya waigizaji chipukizi na kuviendeleza na mambo
mbali mbali ya jamii na tasnia ya filamu na muziki.
“Kwa
njia hii, jamii itaendelea kumkumbuka kila siku na si kusubiri
maadhimisho ya siku yake aliyokufa tu, siku hii (Aprili 7 kila mwaka)
itabaki kuwa ya kukumbukwa, lakini tutajihusisha na mambo mengine ya
maendeleo na kusaidia jamii,” alisema Mtegoa.
Alisema
kuwa wameamua kuipa jukumu kampuni ya Vannedrick Tanzania Limited
kufanya shughuli za uzinduzi wa taasisi hiyo kutokana na uadilifu wao na
kuvunia na jinsi inavyojihusisha na mambo mbali mbali katika jamii.
Mkurugenzi
kuu wa Vannedrick Tanzania Limited Frederick Mwakalebela alisema kuwa
siku hiyo mbali ya kuwa na Red Carpet, pia kutakuwa na burudani mbali
mbali za muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya na vichekesho kutoka
kwa wasanii maarufu hapa nchini.
…..
alisema kuwa kutakuwa na maonyesho ya filamu mbali mbali za marehemu
Kanumba ikiwa pamoja na script alizokuwa akiandika yeye mwenyewe, nyimbo
alizotunga na vingienvyo.
“Pia
kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Movie ambao wameanza
maandalizi kwa ajili ya siku hiyo maalum kwa waigizaji na mashabiki wa
filamu nchini, tunawamba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha siku
hiyo,” alisema


Post a Comment