Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga
kwa tiketi ya chama hicho,Ndugu Godfery Mgimwa,wakati wa mkutano wa
kufunga kampeni katika jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Kidamali kata
ya Nzihi,Iringa Vijijini mkoani Iringa.Uchaguzi wa jimbo la Kalenga
unafanyika kesho siku ya jumapili,Machi 16,kuziba pengo la aliyekuwa
Mbunge wa jimbo hilo,Waziri wa Fedha na Uchumi,Marehemu Dk.William
Mgimwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia Wananchi wakati wa kufunga Kampeni
za Uchaguzi wa jimbo hilo jioni ya leo,katika kijiji cha Kidamali,kata
ya Nzihi Iringa vijijini.
Mkutano wa kufunga kampeni ukiendelea kwenye kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi jioni ya leo.
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke
wake,Bi.Robby Mgimwa kwa wananchi wa kijiji cha Kidamali kata ya
Nzihi,ambako kumefanyika mkutano wa kumfunga kampeni jioni ya leo.
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu Mgimwa akiwa amebebwa juu
juu na Wafuasi wa chama hicho,mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa
kufunga kampeni za cha hicho,zilizofanyika katika kijiji cha
Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa vijijini.
Mbunge
wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe akihutubia mbele ya wananchi
katika suala zima la kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM,Jimbo la
Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kidamali
Kata ya Nzihi Iringa vijini.
Mke
wa Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Bi Robi
Mgimwa akiwa amepiga magoti mbele ya wananchi waliokuwa wamefika kwenye
mkutano wa mwisho wa kampeni za chama hizo,akimuombea kura mumewe ili
ashinde.
Wakina dada wakifuatilia mkutano huo
Wadau nao walikuwepo.
Wananchi
mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya lala salama ya CCM,jioni
ya leo kwenye kijiji cha Kidamali,kata ya Nzihi Iringa Vijijini.
Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa kampeni.
Wakazi wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi wakishangilia jambo.
Niabu
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akimnadi na kumwombea kura
mgombea wa Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu Godfreya Mgimwa katika
kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi,katika mbio za kufunga mkutao wa
Kampeni jioni ya leo
Mke
wa Mgombea,Bi Robby Mgimwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana,kushoto ni Katibu wa CCM mkoa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mhadhiri wa chuo cha
Tumaini na Mtangazaji wa Radio One na ITV,Godfrey Gondwe.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha
Kidamali,Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini jioni ya leo,kabla ya kuhutubia
kufunga kampeni za chama hicho,kupisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
hapo keshoi katika jimbo la Kalenga.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga (CCM),Ndugu
Mgimwa wakiwapungia mikono wananchi jioni ya leo kwenye mkutano wa
kufunga kampeni za chama hicho.
Post a Comment